SERIKALI NA TAASISI ZISIZO ZA KISERIKALI ZATAKIWA KUFANYA KAZI KWA UWAZI.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ( Utawala Bora) Mh Kapt. (mstaafu), George Mkuchika akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa uwazi na kusikilizana kati ya Serikali na taasisi zisizo za kiserikali barani Afrika mkutano uliofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.



Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Issah Mwambene akichangia kwa upande wa serikali kuwa serikali ya Tanzania ni sikivu, wakati wa mkutano wa Uwazi na usikivu katika mambo ya uchumi serikalini pamoja na taasisi zisizo za kiserikali katika bara la Afrika.



Mkurugezi wa kampuni ya Compass Communications Ltd Maria Sarungi akizungumza katika mkutano wa Uwazi na Usikivu uliowakutanisha wadau mbalimbali kutoka bara la Afrika, mkutano hup umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.




Mkurugeni Mkuu wa TWAWEZA Aidani Eyakuza akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika kufunga mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali kutoka Bara la Afrika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.



Baadhi ya Wadau wa mkutano kutoka nchi mbalimbali za Barani Afrika walihudhuria mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.

SERIKALI NA TAASISI ZISIZO ZA KISERIKALI ZATAKIWA KUWA WAZI.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Serikali na Taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali Barani Afrika zimetakiwa kubadili maudhui yake kwa kuweka mipango ya uendeshaji wa mambo yake kwa uwazi hasa kwenye sekta za uchumi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ( Utawala Bora) Mh Kapt. (mstaafu),George Mkuchika wakati akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali Barani Afrika kutoka serikalini na Taasisi zisizo za kiserikali,mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijijini Dar es Salaam leo.

Mkuchika amesema kuwa,mkutano huo utasaidia sana endapo yaliyozungumzwa kwa siku mbili katika mkutano huo yatafuatwa na wananchi wataweza kujua mambo mbalimbali katika nchi zao, pia kila mwananchi ashiriki vyema kufanikisha malengo ya nchi.

Pia kwa upande wa serikali amesema kuwa serikali ikiweka mambo yake kwa uwazi pia inaweza kukosolewa, sio kila jambo inalofanya ni sahihi inahitaji kukosolewa ili kuleta maendeleo, pia wananchi waweze kufahamu nini kinaendelea katika nchi husika.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company