Abu Al Anas Al Libi gaidi wa Al Qaeda anadaiwa kuongoza mashambulizi ya kigaidi 1998 katika Ubalozi wa Kenya na Tanzania
www.longwarjournal.org
Majeshi ya Marekani yamefanikiwa kumtia kizuizini Mshirika wa Alqaeda ambaye anahusishwa na mashambulizi ya kigaidi ya mwaka 1998 katika balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania.
Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon,George Little amebainisha Abu Anas Al Libi kwa sasa anashikiliwa kisheria na jeshi la Marekani baada ya muendelezo wa operesheni za Marekani dhidi ya ugaidi na kwa sasa yuko kizuizini katika eneo moja nje ya Libya.
kiongozi huyo wa kijeshi alikaririwa akizungumza katika kituo cha televisheni cha CNN kuwa operesheni ya kumkamata mtuhumiwa Libi linakibali na kutambulika kwa serikali ya Libya ingawa Vyombo vya usalama vya nchini Libya vikidai kutotambua tukio lolote la kutekwa au kukamatwa kwa mtu yoyte.
Ripoti ya kukamatwa kwa mtuhumiwa Libi ni sehemu ya operesheni maalum ya majeshi ya marekani ambapo kuna taarifa kuwa maesji ya Marekani pia yameshambulia makazi ya kiongozi mwandamizi wa kundi la kigaidi la Alshabab kusini mwa somalia ingawa haijabainishwa kama aliuawa au alitekwa.
Serikali ya Marekani ilitangaza donge nono la kitita cha dola za Marekani milioni 5 kwa yoyote ambaye amgefichua alipo gaidi Libi ambye alitajwa katika orodha ya magaidi yanayowindwa na marekani ambaye jina lake rasmi ni Nazih Abdul Hamed Al-Raghie.
Hayo yanajiri wakati jana jumamosi kundi la wanamgambo la alshabab likiarifu kuwa kumekuwa na mashambulizi yaliyofanywa na jeshi maalum la mataifa ya Marekani,Uingereza na Uturuki katika makazi ya kiongozi wa kundi hilo huko kusini mwa Somalia,taarifa ambayo Uingereza imakanusha kuhusika katika shambulizi hilo.www.hakileo.blogspot.com
No comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA