Pages

Tuesday, October 8, 2013

Matokeo ya ubunge yaanza kutangazwa nchini Guinea leo.


Wapiga kura nchini Guinea

Na Victor Melkizedeck Abuso

Chama Tawala nchini Guinea kinaongoza katika matokeo ya awali ya Uchaguzi wa Wabunge yanayoendelea kutolewa na Tume Huru ya Uchaguzi CENI kipindi hiki Upinzani ukishinikiza kuitishwa kwa uchaguzi mwingine.
Chama cha Rais Alpha Conde RPG kwa mujibu wa matokeo ya CENI kimeshajikusanyia viti 16 kati ya 38 vilivyokuwa vinawaniwa katika uchaguzi huo uliofanyika mwezi uliopita.

Matokeo haya yanatolewa kipindi hiki kukiwa na hofu ya kutokea machafuko nchini Guinea kutokana na msimamo mkali unaooneshwa na Upinzani unaosema kuwa zoezi hilo halikuwa huru na haki.

Chama Kikuu cha upinzani UFDG kimeshinda viti 12, UPR kimeshinda viti 2 huku UPG kikipata kiti kimoja kwa mujibu wa matokeo hayo ya awali.

Kwa ujumla, viti vya ubunge 114 vinawania katika Uchaguzi huo huku viti vingine 76 vikitarajiwa kugawanywa kwa usawa katika majimbo yote nchini humo.

Uchaguzi wa Guinea umekuwa ukiahirishwa mara kwa mara kuanzia mwaka 2010 baada ya Uchaguzi wa rais Conde katika uchaguzi ulionekana wa kuimarisha demokrasia nchini humo.

Mwisho wa uchaguzi wa Ubunge nchini Guinea ulifanyika mwaka 2002 wakati utawala wa Kidikteta Jenerali Lansana Conte, aliyefariki duniani mwaka 2008 baada ya miaka 24 kuwa uongozini

Mapema mwaka huu maandamano makubwa yalishuhudiwa nchini humo hasa jijini Conakry na kusababisha zaidi ya watu 50 kupoteza maisha yao katika makabiliano ya kisiasa.www.hakileo.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA