Pages

Monday, October 7, 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI

MNAMO
TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO ENEO LA UYOLE JIJI NA
MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA JULIUS S/O
MWAMBENJE, MIAKA 23, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA NSALAGA- UYOLE AKIWA NA

BHANGI MISOKOTO 15 SAWA NA UZITO WA GRAM 75. MBINU NI KUFICHA BHANGI
HIYO KWENYE MFUKO WA RAMBO. MTUHUMIWA NI MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU
ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA
JAMII KUACHA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA
NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
MNAMO
TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 23:30HRS HUKO ENEO LA STENDI KUU JIJI
NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA 1. NYELAKOZI
D/O MELANIA, MIAKA 33,,MKULIMA, NA 2. NDAISHIMILI D/O TEONYA,MIAKA
33,WOTE RAIA NA WAKAZI WA NCHINI BURUNDI WAKIWA NA WATOTO 11 AMBAO PIA
NI RAIA WA BURUNDI WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI. MBINU NI
KUSAFIRI KWA NJIA YA KIFICHO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAKABIDHIWE IDARA
YA UHAMIAJI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA
KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWA NI
PAMOJA NA WAHAMIAJI HARAMU ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.

WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]

MNAMO
TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 08:30HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA
MAJENGO KIJIJI CHA LUPA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI
WAKIWA DORIA WALIMKAMATA LYIDIA D/O AMBAKISYE, MIAKA 25, KYUSA,
MKULIMA, MKAZI WA LUPA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI[GONGO] UJAZO WA
LITA 5. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI
AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA
MATUMIZI YA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA
NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].

MNAMO
TAREHE 06.10.2013 MAJIRA YA SAA 09:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA
MAGUNGA KIJIJI CHA MAMBA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI
WAKIWA DORIA WALIMKAMATA JOHN S/O LUTIMBO, MIAKA 29, MSUKUMA, MKULIMA,
MKAZI WA MAMBA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 4.
MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE
MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA MATUMIZI YA
POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI
KWA AFYA YA MTUMIAJI.www.hakileo.blogspot.comm

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA