Tanzania yatafuta washirika wapya nje ya EAC


Serikali ya Tanzania imeanza kutafuta washirika wapya wa kibiashara nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kujitokeza msuguano kati yake na baadhi ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo. Duru za habari zinaripoti kuwa, maafisa wa ngazi za juu wa Tanzania wameanzisha mazungumzo na serikali za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Msumbiji kwa madhumuni ya kubuni ushirikiano wa kibiashara katika siku za usoni. Pia ujumbe wa Tanzania umekutana na maafisa wa Burundi kwa mazungumzo kama hayo. Hii ni katika hali ambayo, Waziri wa Tanzania anayehusika na masuala ya Afrika Masharikli, Samuel Sitta ameliambua bunge la nchi yake kuwa, Dar es Salaam haina budi ila kuangalia mipango mbadala katika masuala ya ushirikiano wa kiuchumi baada ya kuibuka dhoruba kali ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hatua ya Tanzania ya kutafuta washirika wapya nje ya EAC inatokana na kutengwa nchi hiyo na mataifa ya Rwanda, Uganda na Kenya kwenye mradi mkubwa wa kupanua miundombinu miongoni mwa nchi hizo.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company