Pages

Monday, March 17, 2014

Njama ya mashambulizi yatibuliwa Kenya


Mji wa Mombasa umekuwa ukishuhudia machafuko yanayosababishwa na vijana wanaokumbatia itikadi kali za diniPolisi mjini Mombasa pwani ya Kenya wamewakamata watu wawili waliokuwa na mabomu waliyoyatengeneza ndani ya gari lao

Kwa mujibu wa polisi washukiwa hao mmoja raia wa Kenya na mwingine msomali, walikuwa wanajiandaa kufanya mashambulizi katika eneo lisilojulikana.

Inaarifiwa polisi waliwakamata baada ya kupata taarifa kuhusu njama yao.

Vyombo vya habari vinasema kuwa usalama umedhibitiwa mjini humo kufuatia tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA