Miongoni mwa picha inayooneha uhaba wa maji na adha zake |
Wakati raisi
wa awamu ya nne Mh. Kikwete alipoingia madarakani kwa awamu ya kwanza siku
anaapisha baraza lake la mawaziri la kwanza alihaidi kupambana na tatizo la
maji aliloliita ni tatizo sugu.
Kauli ile iliibua
matumaini makunbwa sii kwa watu wa mkoa wa Arusha tuu bali kwa taifa zima kwa
ujumla,waziri wa maji Mh. Jumanne Magembe mara kwa mara amekuwa akikiri kuwepo
kwa tatizo kubwa la uhaba wa maji katika taifa la Tanzania, lakini hakuna jitiada
za kuridhisha zilizo fanyika.
www.hakileo.blogspot.comKwa leo
sitazungumzia tatizo hili kwa ngazi ya kitaifa ila nitagusia sana katika eneo
la Morombo ,Moromba ni tarafa iliopo mkoani Arusha katika Manispaa ya Halimashauri
ya Arusha Mjini.
Eneo hili
lipo pembezoni mwa mjii huu na ni miongoni mwa miji mipya inayoendelea kwa kasi
kubwa.Ila maendeleo hayo ni ya ongezeko la watu na makazi tuu kwani huduma za
kijamii ikiwemo huduma hii muhimu kuliko zote ya maji haiboreshwi.
Nashindwa
kuelewa ni kwa nini serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi ni inakuwa na
kigugumizi cha kutekeleza wajibu huu kwa wananchi
wake,ambao ni miongoni walio kipa ushindi wa kishindo kwenye chaguzi zake hususani ngazi ya urahisi.
wake,ambao ni miongoni walio kipa ushindi wa kishindo kwenye chaguzi zake hususani ngazi ya urahisi.
Kutokana na
adha hiyo wakazi hawa wanalazimika kutumia njia mbadala ili kuhakikisha yakwamba
wanapata maji,jambo ambalo ni haki yao ya msingi ya lazima inayo paswa
kutekelezwa na viongozi wao wakiwemo mbunge wao ambae ni Godbless Lema,madiwani,
wenyeviti wa vijiji na watendaji, pia mkuu wa wilaya na mkoa.
Miongoni mwa
njia hizo mbadala ni uchimbaji wa visima ili kupata maji, ni kweli maji ya aridhini yanaapatikana kwa ukaribu sana
katika eneo hili, ila maji haya yana chumvi na magadi mengi hali inayo ya fanya
ya sifae kwa matumizi ya kunywa na kupikia.
Hata
watalamu wa maji kutoka idara ya maji hawa liruhusu hilo kutokana na madhara
yanayo weza kusababishwa na matumizi ya maji hayo.
Lakini kwa
kuwa shida haina adabu watu hulazimika kuyatumia kwa matumizi hayo yasiyo
ruhusiwa, vya kula vinavyo pikwa na maji hayo hupoteza ladha yake na kubadilika
rangi.
Mfano ugali
huwa na rangi ya njano pamoja na wali nao pia huwa mlaini sana kutokana na
magadi (hupondeka/mabokoboko).Huwezi kupika chai bila kuweka viungo vyenye
harufu kwani licha ya maji hayo kuwa magadi
na chumvi pia yana harufu ambayo huusika katika kupoteza ladha.
Kwa wanaolazika
kunywa maji hayo basi hawayaruhusu kutua kwenye kinywa badala yake huya meza moja
kswamoja tena kwa kasi iliyo kubwa.
Magonjwa ya
taifodi na homa za matumbo ni magonjwa ya kawaida kwa wakazi hawa, amweba na
minyoo ni miongoni mwayo pia.
Maji haya hayapatikani kwa urahisi kutokana na idadi
kubwa ya watu,kwa waliobahatika kupanga kwenye nyumba zenye huduma hiyo basi
kwao ni hauweni kubwa ila kwa ambao sivyo hulazimika kunununa ndoo moja ya lita
ishirini kwa shilingi 50/= na wengine kutokana na ugumu wa maisha hulazimika
kuchota usiku au kuvizia wakati ambao mmiliki au wa husika hawapo ili waweze
kuteka maji hayo, mbinu hiyo ambayo sii sahihi huwezekana kwa visima ambavyo
havi+fungwi na kofuli.
Eneo hili
lililotelekezwa kimaendeleo na serikali lakini lenye kupendwa na wakazi wengi
kutokana na ukaribu wake na maeneo wanayofanyia shuhuli zao za kila siku lina
bomba chache za maji safi ambayo husambazwa na idara iliyopewa dhamana na
serikali.
Licha ya
bomba hizo kuto kukidhi maitaji ya utitiri huwo wa watu baya zaidi maji
hupatikana kwa msimu.Kwa kawaida bomba hizo huwa na huduma ya maji hayo mara
mbili kwa wiki au moja lakini wakati mwingine hususani vipindi vya kiangazi
hutoa maji mara moja kwa mwezi na mwaka jana wakazi hao waliwai kukaa miezi
mitatu bila huduma hiyo na halikuwa jambo la ajabu kutoka kwa viongozi walio
kabidhiwa dhamana na wakazi hao ya kutekeleza wajibu huo
Nimewai
kushuhudia fujo mara nyingi kwenye bomba hali inayotokana na uhaba wake; ukija
kwenye eneo hili usingae kuwaona wanawake wakiwa na watoto migongoni na wanaume
wenye ndoo mikononi na vichwani na wengine kwenye mikokoteni wakikimbilia
boombani.Mji haya wameyabatiza jina na kuyaita maji m ya kunywa wakiwa na
mantiki ya kwamba huyatumiki kwa matumizi ya kuogea wala kufulia.
Katika
kutatua tatizo hili nimefanya jitihada kadha ili kuondoa kadhia hii,kwa bahati
mbaya jitihada zote zimekuwa ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu au kufukuza
upepe na sitamshangaa atakae zifanananisha na kazi ya kupaka upepo rangi ama
adhabu ya kutafuta samaki aliye hai kwenye vumbi.
Kwanza
kabisa nilianza na mbunge wa jimbo hili ambae ni G. Lema,nilienda ofisini kwake
mara kadhaa lakini siku mkuta labla kutokana na majukumu mengineyo, kwa
kuwanilikuwa na barua mkononi mwangu iliyojaa masahibu haya niliamua kupitisha
chini ya mlango wa ofisi yake.
Licha ya
barua nimewahi kuwasiliana nae mara kadhaa kwa njia ya simu huku nae akikiri
swala hilo kuwa sugu na kuandaa maandamano ambayo baadae yaliota mbawa yaani
hayakufanyika.
Kwa mkuu wa
wilaya pia nilienda licha ya kuacha barua pia nilikutana nae ana kwa ana cha
ajabu alikiri tatizo lipo ila akanitaka nikakusanye saini za wakazi ili
adhibitishe kama kweli ni wao wamenituma, siku elewa mantiki ya kauli ile iIa
nili hisi ni njia za kukwepa wajibu kwa kutumia njia za kisiasa.
Kwa mkuu wa
mkoa nilienda pia,kwa mara ya kwanza nilikuwa na nia ya kuonana nae ila katibu
wake alinizuia nami kulazimika kumwachia ujumbe,tatizo lilizidi kuririma ndipo
nilipo amua kurejea tena kwa mkuu huyo wa mkoa,baada ya malumbano ya hoja na
katibu wake yaliyochukua muda kadhaa niliruhusiwa kuonana nae.
Kumbe alijua
fika kabisa hakwepo ofisini, nilipofika sikumkuta yeye wala msaidizi wake
ilinibidi nitoe maelezo kwa kinywa kwa katibu wake wa pili, alibisha ila alimwita
mfanyakazi mwenzake anaeshi eneo hilo, bila kutafuna wala kumungunya maneno
alikiri tena kwa herufi kubwa.
Basi walihaidi kumfikishia taarifa mkuu wa mkoa
name pia niliacha barua iliyo dadavua kwa kina zaidi.
Jitiada hizo
nilizianza mapema mwa mwaka huu lakini hadi sasa hali bado ni tete,mwenyeviti
wa vijiji na vitongoji wameitisha mikutano mara kadhaa ili kulipatia ufumbuzi
lakini jitiada zao ni sawa na zile zangwangu.
Wenye
dhamana husika wana majibu ya kisiasa kwani hujitetea ya kwamba maji ni machache
bila kufikiri ya kwamba mbona maeneo ya mjini Njiro na yana maji ya kutosha
kila siku angali idara inayo sambaza
maji ni moja?
Pia katika
eneo hili kumepitishwa bomba la maji ambalo halikosi maji na linaelekea kwenye
kambi ya jeshi iliopo Olijoro, labla wanajeshi ndio wenye haki ya kupata maji
kuliko wakaazi hawa ila ni kwa nini kisingechimbwa kisima kambini ambacho kitaifadhi maji kwa muda alafu muda
huwo wakazi Morombo wakapewa maji kwa kuifadhiwa pia kwenye kisima chao.
Ninaamini ya
kwamba kila mwaka hutengwa kiasi kwa ajili ya kutatua tatizo hili katika sehemu
kadhaa za nchi yetu lakini changamoto huwenda ikawa fedha hizo hazifanyiwi au hazitekelezi
kusudio na uwenda ufisadi ni sababu kubwa,kwa hiyo serikali kuu hainabudi
kufwatilia na kuhakiki matumizi yake yanahakikiwa na watakaobainika kuhusika na upuzi huwo
wachukuliwe atua za kisheria.
Pia na
muunga mkono waziri husika kwa kauli yake ya kwamba wapo wafanyakazi waidara
mbali mbali hapa nchi ambao hawafanyi kazi zao kwa umakini na hii hutokana na
rushwa au masilai binafsi kutoka kwa watu wanao uza maji , kwani hata huku
Morombo hilo nimelibaini.
Kwa maoni wasiliana nami, simu;0759859287 au
baruapepe; hakileotanzania@gmail.com.