Najua na ndivyo ilivyo ya kwamba watanzania wengi wanaimani na Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa raisi wa kwanza wa hili taifa,na wakati mwingine ukidiriki kutamka adharani ya kwamba Mwali alikosea basi unaweza kupigwa ama kuonekana ni msaliti au mtu aliyekosa uzalendo.
Unajua ukweli ni ukweli hata kama ulifukiwaga hapo zamnani,,na imefika wakati wa watanania kuuukubali hata kama unauma,
Wakati wa Mwalimu Nyerere taifa hili lilikuwa na wakati mgumu sana kiuchumi kuliko kipindi chochote ilicho wahi kupitia,watu walikuwa wakivaa magunai kwa nguo za viroba,huku wakinywa chai isiyokuwa na sukari na wengine wakifulia magadi badala ya sabuni.
Hanii ngii akilini eti mtu unaenda kununua sukari au kipande cha sabuni dukani asubuhi na kulazimika kusubiri hadi saa kumi na mbili jioni ukisubiri foleni kubwa ya wanakijiji wote..Ukiendelea kumtetea huyu mzee tafakari hili maana yamkini jamu ya dakika tano tuu inakukera kwa kuchelewa kazini,,na sababu kubwa eti kuwe na duka moja tuu lakijiji,,UJAMAA,,haukuwa ujamaa ulikuwa ni UFUKARA..
Sera na mfumo wakijinga wa ujamaa uliopigiwa upatu na Mwalimu Nyerere ndio chanzo cha hayo yote,Mwali chakushangaza aliwanyima watu hata kuwa na Tv,embu niambie hilo ni sahihi ? nalo lililinda viwanda vya ndani,watu walikuwa hawaruhusiwi kununu gari au baisikeli bila kibali.
Siku moja Mzee mmoja Rafiki yangu alinunua suti nchini Kenya na alipofika Moshi Mjini askari aliyevalia kikaptula akamsimamisha na kumuuliza umetoa wapi ?
Katika utawala wake aliwadanganya watu eti serikali ni mimi na wewe,,huo ni uongo mtupu,,hatukuwai kuwa na serikali ya aina hiyo labla ile ya Abrahamu Linckon,ila hii ya kwetu ni kwa ajili ya wao wenyewe.
Ukweli ni kwamba Mwalimu aliamini katika jambo amabalo hakulifanyia utafiti wakutosha na ndio maana alikuwa akitapa tapa mara anzishe azimio la Arusha amabalo hata yeye mwenyewe alishindwa kulitekeleza,
Alipoona nchi sasa inamfia akamkabidhi Mwinyi ,Mwinyi baada ya kupokea Taifa lenye viraka akataka kubadilisha nguo kabisa kwenye taifa hili,lakini Mwalimu akaanza tena kumuingilia,sasa swali kama Mwinyi kakosea mbona wewe umekimbi ?
Ukweli nitasema hata kama wewe yamkini ni miongoni mwa watu wanaomsifu Mwalimu bila kukubali mapungufu yake amabayo hata yeye mwenye aliwai kuyakiri,,achakujifanya unamjua zaidi yeye anavyo jijua mwenywe .
Mwinyi nae akamuogopa mzee nadhani alimfahamu alivyo na angeliweza kumchafulia kama alivyo fanya kwa wengine kama wakina Omar Jumbe,Tuendelee ,,Mwinyi baada ya kushindwa kubadilisha nguo,,akaamua kuziba viraka,,Ndipo alipo ruhusu soko huria na kuagiza vitu ama bidhaa kutoka nje ya nchi.
Unajua Mwali alilivika taifa vazi la ujamaa ambalo ambalo hakulitafiti ama hakujua ni lamazingira ya joto au baridi? Jioni au usiku ?,,Pili huyu Mzee aliyekuwa makini sana kuongea na mwenye ucheshi ila mwenye maamuzi ya kuudhi na kuchoma na kuangamiza huku wanaoumia hawajitambui..Alikuwa mbishi kwa kifupi,MWALIMU ALIKUWA AMBILIKI,,
Usikasirike wala sina hila na huyu mzee ila ukweli ndo jadi yangu,aliwahi kushauriwa ya kwamba asipigane vita vya Kagera ambavyo vilikuwa ni vyakutengenezwa ili amrudishe rafki yake mkubwa Obote Madarakani,,ukibisha kamuulize aliyekuwa na dhamana ya fedha wakati huo Mzee Edwin Mtei wala akai mbali ni hapo Tengeru Arusha tuu.
Baada ya kuona ushauri huo ni mzito na ataumbuka akamfukura Mtei na Mtei akapata kazi na kuwa Mkurugenzi wa shirika moja la kimataifa la fedha barani Afrika,,Nyerere kwa kuwa alikuwa na akili nyingi ambazo hakuweza kuzitumia vizuri aliamua kukopa fedha katika serikali ya ZANZNIBAR hali iliyoifilisi nchi hiyo hadi leo..
Tafadhali usinikasirikie ila kama kweli unataka tutoke hapa tulipo ni lazima ukubali ukweli na ukweli pekee ndio utako kuweka huru.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago