HABARI KUU ZA LEO na OSCAR SAMBA
print this page
HABARI NA Oscar Samba
Showing posts with label FIKRA ZA LEO. Show all posts
Showing posts with label FIKRA ZA LEO. Show all posts

WAKENYA NA MAENDELEO,WATANZANIA NA UMASIKINI NA CCM


NIMEITOA FACEBOOK.
Achana na CCM,,,, na serekl Yake,,, inayoendelea kuyafanya,,,,, nimeikuta hii sehem,,,, naamni itazid kukupa point fulan,,,, kweny akil ya mtu anaetaka mabadiliko,,, tofaati ya wakenya na Watanzania Wakenya wanacheza smart games na Watanzania bado tumelala.. After Precision Airlines (PA) kuwa threat kwa operation za Kenya Airways (KQ) route za Tanzania na Kenya, KQ wakaingia ubia na PA very smartly na wakawa wanaihujumu undercover. Leo hii PA iko hoi na tayari Operations za Jomo Kenyatta- KIA, Jomo Kenyatta-Mwl. Nyerere zimerudi kwa KQ... Pili, baada ya TBL kuruhusiwa kuuza bia Kenya, na Kenya walete bia zao Tanzania. TBL wakakaribia kuuwa bia za Wakenya huko kwao wakati huo bia yao TUSKER ikawa haifanyi vizuri hapa Tanzania. Wakavunja makubaliano, ili kila mtu afanye biashara yake kwake. After years EABL ya Kenya ikaingia ubia na SBL na wakaipa License ya kuzalisha na kusambaza TUSKER hapa nchini.. Smartly EABL wanauza hapa kwetu wakati sisi TBL haiuzi kule kwao.. Wakati hayo yote yanafanyika Watanzania tunalazwa na fikra za kijinga za viongozi wetu wa CCM.. Education Matters alot 2004 Tanzania tulikuwa na Ndege mbili za serikali (Air Tanzania) na Kenya walikuwa na Ndege 19 (Kenya Airways-KQ).. 2015 Tanzania tuna Ndege 1 ya kukodi kwa ajili ya kupigia Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Kenya wana Ndege 47 zinazotua katika viwanja 62 vya mabara yote duniani... Tukumbuke bila kuwa na Shirika letu la Ndege Utalii tunaongelea ni kazi bure.. Kenya taratibu inautawala Uchumi wa Tanzania, tayari wana Bank mbili zinazofanya kazi nchini (KCB and Equity Bank), Tanzania bado hatuna Bank yeyote Kenya. Supermarkets za Kenya tayari zimeingia nchini na kuuwa zetu (Nakumat tayari imeshainunua Shoprite (T), UCHUMI Supermarkets).. Sisi Imalaseko Supermarkets zilishakufa kule Kenya. Soko la Hisa Dar Es Salaam (DSE) lina Jumla ya Kampuni 21, kati ya hizo Kampuni 7 ni za Kikenya lakini Soko la Hisa la Nairobi (NSE) lina zaidi ya Kampuni 64 na hakuna kampuni hata moja ya Kitanzania.. Hii ni mbaya sana kiuchumi.. Serengeti National Parks ni mbuga bora iliyoshika namba moja kwa Afrika, na Ngorongoro ikiwa namba 5.. Masai Mara ya Kenya ni namba 8. Lakini pia Tanzania tuna Mlima Mrefu zaidi Afrika Mlima Kilimanjaro ambao pia ni kivutia kikubwa cha Utalii.. Lakini maajabu ni kwamba Kenya wanakusanya pato kubwa sana kwenye Utalii kuliko Tanzania. Mwaka 2013 pamoja na matukio ya kigaidi Kenya ilitembelewa na watalii million 1.4 wakati Tanzania yenye amani tele ilitembelewa na watalii million 1.04.. Amani wanayoihubiri CCM na vivutio vyetu vya Utalii bado havijatufaidisha chochote.. Pato la Mtanzania kwa mwaka ni Tshs. 1,996,000 na Pato la Mkenya kwa mwaka ni Tshs. 3,176,000.. Pato la nchi (Tanzania) ni Tshs. Trillion 98.36 na Pato la nchi kwa Kenya ni Tshs. Trillion 140.. Tanzania kuna madini ya kila aina, Tanzanite, Dhahabu, Rubi, Uranium, Makaa ya Mawe, Chuma, Kenya hawana madini ya aina yeyote lakini bado wametuzidi pakubwa kwenye pato la Taifa.. Sekta ya madini inachangia 3.3% kwenye pato la taifa kutokana na mikataba mibovu uliyowekwa na viongozi wa CCM.. Kiwanda cha General Tyre cha Arusha kilikuwa kinazalisha TYRE bora kabisa za kazi. Kilikuwa na Soko kubwa Afrika Mashariki na kati. Gari zote za Tours zinazotembea porini Afrika Mashariki yote na Afrika ya Kati zilikuwa zinafunga TYRE ya GENERAL. Hata wale wapigana vita za msituni huko Kongo na Sudan walikuwa hawaendi kupambana bila kuhakikisha Land Rover yake imefungwa Tyre ya General. Magari ya serikali yote yalikuwa yanafunga Tyre ya General.. Kiwanda kilikuwa kinalipa kodi isiyopungua Billion 100 kila mwaka.. CCM wakafanya hujuma kukiua, zinatolewa subsidy zinaishia kwenye matumbo yao. Wakenya walivyosmart wakaiba ile Technology ya Tyre za General wakafungua kiwanda chao huko kwao kikaitwa YANA Tyre ambaye sasa ndiye Supplier mkubwa wa Tyre Afrika Mashariki na Kati.. Kampeni zinaanza wamejifanya kuifufua General Tyre, Je, wataweza kupambana na Yana Tyres?? Kenyans are always SMART kuliko akili za CCM CCM wanasema hapa ni Kazi tu.. na kwa mwananchi mwenye akili ndogo atawapigia kura. . IT'S HIGH TIME TO OPT FOR CHANGES
0 Toa maoni yako.

KESHO NITAWEKA MAKALA INAYOSEMA "PRO. LIPUMBA JIANDAE KUITWA MSALITI KAMA ZITTO" Hatua hii imekuja mara baada ya kujiuzulu kwa Pr. Lipumba CUF ikiwa ni masaa machache mara baada ya makala yangu isemayo "CHADEMA inavyoimeza ukawa" Kwa taarifa zadidi tembelea www.hakileo.blogspot.com

HABARI ZETU
0 Toa maoni yako.

CHADEMA INAVYOIMEZA UKAWA.

Na OSCAR SAMBA.
Salamu zangu nyingi kwako ewe uliyemtanzania ama Raia yeyote katika taifa lolote lile duniani,salamu hizi zinawapendelea  zaidi kwa wale wanamapinduzi yakidemokrasia na wapenda Haki.

Ambao kwao ushabiki uliyo chanzo cha upofu kifkra hautajwi kwao.
Siku chache zilizopita nilitoa taadhari kwa uma wa watanzania hususani wale wanaotambua dhana ya
Demoktrasia ya Haki,katika makala yangu niliwataadharisha Chadema kuwa wanapaswa kuwa makini katika Umoja wao wa Ukawa kwani wao ndio wenye nguvu zaidi na wasijaribu kutumia mwanya huo kuwakandamiza wagombea ama wanachama wa vyama vingingine katika ummoja huo.

Ninasikitika kwani sauti yangu haikusikika masikioni mwao,katika makala ile niliwaambia wanachadema kuwa wasikubali kumtoa mgombea Urasi na mwenza wake nikiwa ninahitaji kuwa wau vyama vingine vifanye pia hivyo,ila mambo hayakuwa vile kama nilivyo shauri.

Hali hii inaweza kuwa imechangiwa na wenzano wa CUF kufanya hivyo kule zanzibar kama ndivyo,lakini kihalali ingeitajika kwa upande wa Zanzibar pia kuwe na mchnganyiko wa vyma viwili na huku hivyo.

Kinachoendelea sasa kisiasa kinatafsiriwa kuwa "CHADEMA imeimeza UKAWA"haingi akilini eti Duni awe na uwezo mkubwa kuliko Pro. Limpumba ama Mbatia au Chadema kiwe ndicho chama chenye wagombea wenye nguvu ama uwezo mkubwa kuliko vyama vyote vingi; vitatu yaani NCCR MAGEUZI ,CUF na NLD.

Huu ni ulafi wa madaraka, ndivyo ilivyo katika majimbo pia ukifwatilia mgawanyo wa majimbo ni wazi CHADEMA imevimeza vyama vingine, Sina dhamira ya kuigawa UKAWA ila dhamira yangu ni ya dhati katima kuujenga umoja huu ukizingatia ndio umoja wa kwanza katika historia ya nchi yetu wenye mafanikio makubwa hadi sasa.

Nikukumbushe kuwa katika makala hiyo nilieleze adhari zake ikiwemo kuwakwaza wakina Pro. Lipumba na vyama vingine, hili limeshajidhiirisha,hakika hali hii ikifumbiwa macho nguvu ya UMOJA huu itafifia na kujikuta wanashindwa kutimiza malengo yao hali itakayo ijengea nguvu CCM zaidi.

Tafadhali niruhusu nichukuwe wasaa huu kukumbusha kuwa swala la ulafi wa madaraka ndani ya CHADEMA halijaaza leo kwani miaka michache iliyopita walipoingia bungeni wakiongoza kwenye bunge la Jamhuri kwakuwa na wabunge wengi waliwatenga wenzao na kuunda kambi rasimi bungeni wenyewe.

Sababu walizozitoa zilikuwa dhaifu na hafifu lakini chakushangaza bila kurekebishwa kwa sababu hizo walikuja tena kuunga nawaliowatenga,kwkuw amisingi mikubwa ya Sisasa za dunia siku ya eo ni masila wenzao waliposikia UKAW wakakubaliana nao na hatimae kwa pamoja wakatengeneza mipango.

Binafsi nilipoyasikia hayo yakuwa na mgombea mmoja niliweka taadhari mapema kwani nilifahamu lengo na shabaha iliyonyuma ya pazia mapema ila nilihoji sana iweje wakubaliane mapema hivyo,lakin nilidhani ya kwamba huenda tayari wameshakubaliana kuhusu ama nammna watakavyo wapata wawakilishi katika nji ya usawa na haki isiyo na ujanja ujana.

Ninatumia neno ujanja ujanja kwani haniingi akilini eti kila jimbo limsimamishe mgombea wake kulingana na jinsi chama husika kinavyokubalika zaidi kwenye kata ama jimbo hilo, jambo hili ni gumu na halina haki kwani chama kama NLD ambacho hakina mbunge wala diwani kitapata jimbo gani ama kitapata majimbo na kata ngapi ?

Wakati huu sio wakati wakujitoa kama ilivyo dhamira ya baadhi ya viongozi wenye nguvu latika vyama ndani ya UKAWA ila nikukaa katika meza ya makubaliano wazungu wanaita "Round Table" wakati mnaunda ukawa mlikaa kwa pamoja kwenye meza duara na sasa fanyeni hivyo.

CHADEMA nyie ndio wenye dhamna kubwa katika utanzu wa mgogoro huu jitaidini ili kuunusuru umoja huu unaonekana kuwa na nguvu katika Demokrasia na wale mashabiki wa UKAWA na CHADEMA wasiopenda ukweli ama uwazi nawataka wajifunze kupima hoja na uwazi hata kama unawauma.
0 Toa maoni yako.

TUMIA BUSARA KUTAFAKARI KAULI HIZI ZA DK. SLAA KUHUSU LOWASSA KWENDA CHADEMA



0 Toa maoni yako.

KWA HILI LA LOWASA UKWELI NI KWAMBA,CHADEMA IMEPOTEZA WANACHAMA WAZALENDO NA KUJIZOLEA MASHABIKI













Ukweli ni mzuri hata kama huupendi ama hauendani na Fikra zako,hakika CHADEMA imefanya kosa la kiuaminifu na kujipatia faida ya ushabiki na umati wa watu.

Na hasara kwamba imepoteza Imani yake kiuaminifu ambayo ilikuwa miongoni mwa wanachama na watu wenye mapenzi mema na Cha hicho.

Hotuba ya Mbowe ya jana kwa mtu aliye makini alitambua fika kwamba Lowasa amepokelewa CHADEMA sio kwamba anawezo mkubwa ama ametakasika kikashifa ila kwa sababu ni mtu mwenye watu wengi na sifa ama azima yao kubwa kama CHADEMA ni kupata watu wengi.


Kauli kama hii ukiitafakari kifilosofia unapata mantiki nzuri sana,ninayo mengi sana ya kuongea ila kwa leo sitakuchosha kwani makala ninyoianda haijakamilika ila ukweli ni kwamba CHADEMA imepoteza wanachama wazalendo na kujizolea mashabiki ambao ukweli ni kwamba wanafwata upepo tuu.


Nawamepoteza wazalendo wakindaki ndaki ambao mara zote walikuwa wepesi kuamini kilichokuwa kikisemwa na chama hicho juu ya CCM na Mafisadi,

Kwa mtaji huu ukweli ni kwamba watuhumiwa wote wa Ufisadi CCM wakihitaji kuja CHADEMA watapewa nafasi.

Madhara ya ushamba huu kisiasa hayawezi kujitokeza leo ila wakati na wasaa waja ndipo niyasemayo yatakuwa adhairi.
0 Toa maoni yako.

KATUNI YA LOWASA KWA UKAWA


0 Toa maoni yako.

katuni ya kipanya yatoa mwanga kwa ilani ya CCM


0 Toa maoni yako.

KATUNI NA SIFA ZA URAIS


0 Toa maoni yako.

KATUNI; KIPANYA AZIDI KUMCHOKOZA MEMBE

0 Toa maoni yako.

TATIZO NI FIKRA !!!



0 Toa maoni yako.

MIGOMO NI MATOKEO YA SERIKALI DHAIFU na OSCAR SAMBA.

Pichani ni Morogoro, siku ya kwanza ya mgomo wa madereva. Inanikumbusha miaka ya 80 katikati kabla ya ujio wa daladala. Kulikuwa na shida kubwa ya usafiri dar. Serikali ikaruhusu kuingiza nchini magari ya wazi kwa ushuru mdogo. Watanzania wengi waliokuwa diaspora na hata waliokuwa wakirudi nchini walikuja na pickups zao.Picha na Mjengwa
Nayanena haya huku leo hapa jijini Arusha kukiwa na mgomo wa wafanyabiashara hali inayosababisha maduka mengi kutokufunguliwa na watu kukwama kupata mahitaji yao huku swala hilo likiwa na adhari mabaya kiuchumi.

Sina dhumuni la kukupa habari za mgomo wa leo ila nikukumbushe pia siku chache zilizo pita madereva nchi nzima waligoma na kumekuwa na mfululizo wa migomo katika taifa hili.

Ukweli ni kwamba migomo husabishwa na kutokuelewana baina ya pande kuu mbili huku mara nyingi ikiwa ni mamlaka yenye dhamana husika ya usimamizi ikiwemo serikali.
Mfano mgomo wa madereva na wafanya bishara uosababishwa na TRA a mamlaka za juu za serikali kuto wasikiliza wahusika.

Ni ukweli usiofichika kwamba serikali yetu inatabia ya kudharau na kupuuzia malalamiko inayopewa kutoka kwa wafanyakizi ama wannchi kwa ujumla na huu ndio udhaifu ninao uzungumzia hapa.

Wito wangu kwako Rais Kikwete, hakikisha ya kwamba unafanya kazi kwa niaba ya wananchi wako na sio kundi au jamii fulani, Kwa mfano wapo watanzania wanaodai ya kwamba gharama wanazotozwa madereva ni mbinu ya serikali yako kujipatia fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa kisiasa mwaka huu ili chama chako kipite tena.

Nikukumbushe kwamba rais wa Marekani wa 16 Ndugu Abraham Linkon aliwahi kusema ya kwamba serikali nzuri ni ile inayofanya kazi kwa niaba ya wananchi walio wengi.
0 Toa maoni yako.

KATUNI, LOWASA vs MEMBE.


0 Toa maoni yako.

FIKRA ZA LEO,USIWAZE TATIZO BALI WAZA NJIA ZA KUTATUA TATIZO,Na Oscar Samba

Katika hili nawataka ndugu zangu kutokuwaza jambo lolote ambalo linakutatiza bali waza njia za kutatua matatizo,Mfano huna fedha haipaswi kuwaza kutokuwa na fedha ama hitaji lako bali waza njia ambazo zitakazo kuwezesha wewe kupata fedha ikiwemo kuajiriwa,kujiajiri ama njia yoyote iliyonyofu.

Ndoa yako ina matatizo, usikubali kuwaza matatizo kwani utapata ugonjwa wa Moyo bure na kuna hatari ya kuvunja hiyo ndoa, bali waza njia za kutatua matatizo yanayokuzingira katika hayo mahusiano.

MUNGU AKUPE UVUMILIVU KATIKA UNAYOYAPITIA.


0 Toa maoni yako.

FIKIRA ZA LEO: KATUNI YA MEMBE SWAL LAURASI NA MACHAFUKO AFRIKA KUSINI


0 Toa maoni yako.

FIKRA ZA LEO: MAKONDA WA DALALA NAO WAENDE VETA.


Naongea haya kwani leo asubuhi nikiwa katika usafiri wa umma kondakita alitaka kumpakia abiria angali gari lipo barabarani ila dereva wake akamkemea na kumwambia kuwa hauni gari lipo barabarani ngoja kwanza nipaki gari.
Nikatafakari kwa kina nikafahamu kuwa, kumbe madereva wamesomeshwa na wakakubali kusoma kwa  hiyo wanafahamu maadili ya kazi yao vyema.
Ila makondakita hawajapelewa shle na wala hakuna sheria au kibali maalumu kwao kinachowataka wafanye hivyo.
Kwa hiyo naitaka serikali iwapeleke makondakita wote waende shule, kwani wakifanya hivyo watasaidia kujua maadili yao hata katika uvaaji kwani wengi wao wanavaa mavazi yasiokuwa na maadili na lugha zao pia sio njema.kwa hiyo shule itawapa maadili yao yote ikiwemo kuwafundisha sheria zote za usalama barabarani.

0 Toa maoni yako.

KATUNI NA DHANA YA MKAPA YA UWEKEZAJI

0 Toa maoni yako.

TAFAKARI KWA KINA KIREFU HUU UJUMBE WA WAREMA MWANASHERIA ALIYEJIUZULU

0 Toa maoni yako.

KATUNI YA KIPANYA KWA CHAMA CHA ACT

0 Toa maoni yako.

PICHA HII IMENIHUZUNISHA SANA, TUNACHO CHA KUFANYA, TUFANYE SASA..Ni ukatili kwa mtoto Alibino aliyekatwa kiganja cha Mkono Jumamosi.


Ndugu zangu,

Imenihuzunisha sana. Imenisikitisha sana. Haya ya mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi yanachangiwa na kitu kimoja tu; Ushirikina.

Pichani ni mtoto Baraka Cosmas Rusambo mwenye umri wa miaka sita mwenye ulemavu wa ngozi (Albinism). Amekatwa mkono wa kulia katika tukio lilitokea Jumamosi usiku tarehe7 Machi kwenye kijiji cha Kiseta, wilayani Sumbawanga vijijini, mkoani Rukwa.

Nani anayafanya haya?

Ni watu wenye kuendekeza imani za kishirikina ndio wenye kupelekea aibu hii kwa nchi yetu.

Nini cha kufanya?

1. Mbali ya kuwasaka wahusika wa moja kwa moja. Tuna lazima pia ya kuangazia mazingira yenye kupelekea haya. Hapa kuna umuhimu sasa kwa vyombo vyenye mamlaka kuweka adhabu kali kwa vyombo vya habari vyenye kueneza taarifa zenye kuchochea wanajamii kuamini na kuendekeza ushirika. Vyombo vya habari vyenye kupigia debe mambo ya kishirikina vikutwe na adhabu kali vikithibitishwa kwa ushahidi. Katika hili , kuna vyombo vya habari, kupitia taarifa zake za mambo ya kishirikina redioni, kwenye runinga na magazetini vimetokeea kutengeneza faida ya kifedha huku jamii ikizidi kuangamia kwa kulowekwa kwenye dimbwi la ujinga. Katika kundi hili, wamo pia waandaaji wa filamu zenye maudhui ya kishirikina bila kutoa ujumbe wa kupambana na imani hizo, bali kuziamini. Badala, yake, vipewe nguvu na hamasa, vyombo vya habari vyenye kujibidiisha na kuielimisha jamii kuondokana na haya ya ushirikina na abrakadabra.

2. Vyombo vyenye mamlaka vianze kazi ya kuwasaka waganga wa kienyeji wenye kufanya kupiga ramli ambazo mara nyingi zimepelekea watu kuelekezwa kutafuta visivyowezekana bila kutoa roho za wanadamu wenzao.

3. Mamlaka husika, viangazie na kutoa adhabu hata kufungua nyumba za ibada, kwa baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini na wamiliki wa nyumba za ibada ambao nao hushiriki katika kuwaaminisha waumini wao juu ya haya ya ushirikina na abrakadabra. Tuifanye kazi hiyo sasa. Haya ni mapambano muhimu kwetu kwa sasa. Tushirikiane.

Maggid Mjengwa.

Dar es Salaam.

0754 678 252(P.T)
0 Toa maoni yako.

FIKRA ZA LEO: WOTE TUHUSKE KATIKA KULETA MABADILIKO,KURA YAKO NA MAAMUZI SAHIHI NI NJIA KUU.

Kumekuwa na wimbi kubwa la watanzania wanao hitaji ama kutaka mabadiliko ya kimaendeleo lakini ukiwatazama kwa umakini utagundua ya kwamba hawataki kutimiza wajibu wake.
Wengine huitaji maendeleo ya maji,barabara na umeme pia pamoja na elimu lakini hao wanakuwa ndo wakwanza kukataa kupiga kura ama waopiga kura humchagua mt kulingana na itikadi yake ya chama,undugu au dini yake.
Fikra za leo zinakutaka kuwa makini katika kulera mabadiliko kwani kama unahitaji mabadiliko kuwa sehemu ya kuyaleta na sio kunungunika na kukaa vijiweni huku ukitupa lawama kusiko husika,acha uvivu wakimawazo chapa kazi fwatilia na jua mambo vizuri.


0 Toa maoni yako.
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company