SOMO LA PASAKA: MAJIRA YA KUJILIWA (KUTEMBELEWA) NA MUNGU.

MAJIRA YA KUTEMBELEWA NA MUNGU
Naam kwa tabasamu mwanana lifananalo na lile lililomkuba BWANA yetu YESU KRISTO pale msalabani mara pazia la Mbinguni lilipo pasuka na Kunene yote yamekwisha; na kukaribisha katika mkala hii tamu na mwanana ewe mteule wa Ufalume wa Mbinguni.
Katiak siku ya leu muhimu kwetu na ufalume wa mbinguni siku ya PASAKA ambayo tuaminio katika KWELI ile KUU ni siku ya kuamdhimisha kufufuka kwa BWANA yetu YESU MNAZARETHI.Ujumbe huu ummetolewa masaa machache yaliyopita katika kanisa la Kiroho lililopo hapa mkoni Arusha eneo la Morombo kanisa la VICTORY CHRISTIAN CENTRE T.A.G  (VCC) na mwangalizi mkuu katika eneo hili la makanisa ya T.A.G.
Makala yetu ya leo inalenga kukuabarisha majira ya kujiliwa kwetu na MUNGU wetu,Msingi mkuu wa neno tunaupata katika kitabu cha Luka 19 -41 tunaona pale Yesu anazungumzana na jiji la Yerusalemu kwa kutokutambua majira ya kujiliwa kwake.
Mungu anasema ya kwamba haya ni majira ya kujiliwa kwa kanisa lake sasa na haitakuwa kama Yerusalemu ambayo haikutambua ila wewe utatambua.
Utakuwa kama  watu wawili ambao walitambua akiwemo Zakayo na Batimay o katika Marko 10.
Katika ijuma kuu wafu walifufuka, miamba ilipasuka wanathailojia wanaamini ya kwamba watu hawa walienedelea kutembea mijini hadi pale Yesu alipofufuka na kwenda nae katika Yerusalemu mpya.
MAANA NA MAKUSUDI YA KUJILIWA NA MUNGU.
KUTEMBELEWA NA MUNGU; ni kipindi maalumu katika wakati ambacho Mungu humjilia mtu na kumtembelea mtu binafsi au kikundi cha watu kama kanisa au familia,kabila ,ukoo au Taifa na Mungu hufanya hivyo kwa kusudi maalumu.
Mungu huchaguwa mwenyewe katika kalenda yake,kwahiyo wewe mwenyewe kama mtu binafsi huweza kutembelewa na Mungu au familia yako.
Mungu alokusudi maalumu lakukutembelea.
KUSUDI LAKE
Yapo mambo makuu matano ambayo ningalipenda kukujuza siku ya leo amayo huwakilisha makusudi haya mema ya MUNGU kwetu.
1.Ili kuwa na ushirika nasi,mwanzo 3:8 Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu akitembea bustanini wakati wa jua kupunga.Mungu alihitaji kutengeneza au kuimarisha ushirika na watu wake.Mungu akitembea na wewe katika ulimwengu huu atafanya mapito yako kuwa mepesi na kufanya maisha yako yasiwe ya kawaida.
Ona mzee kama Zakayo anapanda juu ya mtii,nae alifanya jambo ambalo sio lakawaida Ufunuo wa Yohana sura ya 3,ukisoma utaelewa zaidi.Kumbuka kitabu hiki ni kwa ajili ya watu wanaomjua yeye ndio maana kinaitwa Ufunuo,kumbuka katika kkujiliwa kwako Baraka ya kwanza ni Mungu kuwa na ushirika na wewe.
2.Ili kutukomboa katika hali na mazingira ambayo huleta mateso,kama yale ya wana wa Iziraeli kule Misri,Kutoka 3:7-8  Bwana akasema hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko misri, name nimekisikiaa kilio chao kwa sababu yya wasimamizi wao; maana na yajuua aumivu yao 8 nami nimeshuka iliniwaokowe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka katika nchi ile hata nchi njema kisha pana;nchi ijaayo maziwa na asali hata mahali pa Mkanani ,na Mhiti na Mwashori na Mperizi na Mhivi na Myebusu.
Sisi sote katika maisha ya Kikirito yatupasa tupietie katika majaribu,imani yetu inapojaribiwa Mungu hutuwezesha kupita,fahamu ya kwamba majaribu sio kituo cha kudumu bali ni kituo cha Muda na haikukusudiwa kuwa sehemu ya kudumu kwahiyo usikubali kukata tamaa.
Ingawaje jaribu huweza kudumu kwa muda mrefu ila sio la milele na jaribu hilo linapokuwa ni la muda mrefu maranyingi hugeuka na kuwa mateso ila usikubali kukata tamaa kwani Mungu amejianda kukutembelea kama alivyo mhaidi Ibrahimu ya kwamba watu wako watakaa katika nchi ya ugeni miaka mia 400 lakini nitawatoa.
Mungu anayajua maumivu yako pia anayajua mateso yako tabu ambazo mtu hawezi kuyaona yeye anayajua ndio maana ameweka wakati wake wakukujilia na ukifika nayang’oa kama gr’eda.
3.Ili kutupiganiia. Joshua 5:13 Ikawa hapo Yoshua lipokua karibu na mji wa Yeriko  akavua macho yake na kuangalia  na tazama mtu mume akasimama mbele yake naye alikuwa na upanga wazi mkoni mwake ; Yoshua akaamwendeeaa na kumwambiaa Je! Wewe huu upandde wetu au upndde wa adui zzetu?
Ukiendelea utaona jinsi ambavyo Mungu aliutana nae na hakua adui wala jitu baya.Yoshua katika mazingira haya alikuwa akikabiliana na majaribu na mapamabano makubwa mno,mji waliokuwa wakikabiliana nao ulikuwa na ulinzi mkubwa sana ila Mungu hakumwacha.
Mung alimwamnia Yoshua awe na moyo mkuu awe na moyo wa ujasiri nawe usiogope,Jifunze ili ushicheke na mtu anaetaka kukuangamiza,mtu anaetafuta hatima yako,usikubali kucheka nae na  MUNGU wa Yoshua atakupigania ondoa hofu.
Kwa mamala ya jina la YESU nakutangazia ya kwamba vita hivyo sio vyako bali ni vya BWANA,kumbuuka Mungu hujitokeza ili atupiganie.
4.Kuburudishwa. Matendo ya Mitume 3:19 Tubuni basii ili nije zipate nayakti za kuburudishwa kwa kuwepo kwake BWANA. Baada ya mapito ni mapumziko.
Hata wacheza mpira huwa na muda wa mapumko,Mungu ameweka majira ya kutupooza, ya kutufuta jasho,ni wakati wakunyamazisha maadui zako,huku ukipata wakati wakuburudishwa.Kuna mambo makuu matatu hapa;
(a)  Mungu huleta uamsho na kuleta au kurejesha tumaini na furaha yako ya awali.
(b) Waebrania 4:1,6 Mungu hapa huleta pumziko,ipo siku inakuja ambapo chakula haitakuwa mgogoro,,utaanza kufikiria juu ya mafuta ya gari au sehemu ya kujenga.
(c)  Nyakati za urejesho,Mungu hurejesha vilivyo potea, 1samweli 30:18-19 Utasoma na kuona Daudi alivyokuta ameibiwa ,ila Mungu wa Daud atakurejeshea vilivyo potea ya mkini ni,mali au watoto.Kama alivyo mrejshea Ayubu nawe wakati wako waja,Miaka iliyoliwa na nzike itafidiwa;amina. Soma zaidi hapa Ayubu 42:10.
5.Mungu hututembellea ili kutujulisha hatima yetu,2samwli 7:1 Utaona; Bada ya Mungu kumpa amani Daudi kwa kumshindia madui zake Daudi alitafakari jinsi ya kumjengea Mungu nyumba,pia utaona jinsi Mungu alivyokuja kusema dhidi ya hatima ya maisha yake miongoni mwa hayo alikwepo Sulemani,Mungu alifanya nae ahadi ilikuja kumtoa mtawala wa milele ambae ni Yesu Kristo.Zaidi unaweza kusoma, Yohana 21,Matendo 29.
MUNGU HUTUTEMBELEA ILI UTUONESHA HATUA ZA MAISHA.
Tafadhali kwa mwendelezo wa makala hii usiache kututembelea leo alasiri ili upate mwendelezo wa habari hii NJEMA,,nakutakia PASKA NJEMA na MUNGU wangu AKUTANE NA HAJA YA MOYO WAKO; Amina.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company