Hapa Anamwelezea Alivyokuwa...
- Aliwachachafya maprofesa Mlimani
- Alikwenda Vita Ya Vietnam Na Msumbiji
Ndugu zangu,
Moja ya bahati kubwa kwenye ' Kijiji Cha Mjengwablog' ni ukweli, mmoja wa wajumbe wa Mwenyekiti wenu alipata kusoma pale Chuo Kikuu cha Mlimani wakati mmoja na akina Yoweri Museveni. Mjumbe wangu hapendi kutambulishwa kwa jina lake halisi ( Ninalo kwenye mkoba wangu). Anapenda aitwe BAP- Born Again Pagan.
Hapa anasimulia habari za Museveni aliyemfahamu. Bila shaka kuna maarifa mapya unaweza kuyapata...
"KWA wale wenye kupenda kumjua Yoweri Kaguta Museveni,
mwanafunzi wa Mlimani, someni yafuatayo:
Yoweri Kaguta Museveni alijiunga Mlimani kutokea Uganda, kama
mwanachama wa UPC Youth League. Pengine ndio sababu ya kuwa
karibu sana na TYL. Alichukua BA (General) ya 3:2:2 (Historia,
Sayansi ya Siasa na Uchumi) mwaka wa kwanza. Ali-"drop" Historia na
kumalizia na hayo mengine mawili.
Wanafunzi wote wa ki-Tanzania waliokuwa wanachukua Science
iliwabidi wachukue pia Elimu, na wale ambao walikuwa wakichukua
Elimu iliwabidi wote wamalizie na 3:3:3!
Nilikutana na Yoweri Museveni mwaka wa kwanza katika
somo
la Historia, chini ya ma-Prof. Walter Rodney (Imperialism and
Colonialism); Isaria N. Kimambo, Arnold Temu na John Illife (The
Comparative Analysis of the Rise of Nationalism: Tanzania, Ghana,
India, and China), Terence Ranger (The Rise of the Industrial State:
Britain, Russia and United States), John Illife (Disintegration and
Integration of African Societies: The Role of the Educated Elites) na
John Sutton (Mambo ya Kale – Archaeology).
Museveni na wembamba wake alikuwa "a recluse" (mpweke). Mtu
yeyote asingeweza kuyajua yaliyokuwa akilini mwa Yoweri Kaguta
Museveni! Lakini aliweza kujitoa kwenye cacoon (uzimzinga) na
kuanza kutetea msimamo wake. Alikuwa mwenye machachari mbele
ya ma-Profesa na waadhiri aliowaona kuwa wa upande wa mkono wa
kulia au hawakujua walichokuwa wakifundisha.
Kama profesa/mwadhiri hakujua anachosema (au ni wa mkono wa
kulia sana), Museveni aliweza kutoka nje ya mdahalo na kuwaita wale
ambao aliwafikiria ni "ma-komrade" wake na kusema, "And you (na
kutaja majina) are still sitting there!"- Itaendelea kesho jioni...
NA MJENGWA
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago
+ Toa maoni yako. + 1 Toa maoni yako.
Natamani kujua michapo ya Born again Pagan akiwa UDsm .