Wahamiaji kutoka Afrika wakiwa wameokolewa na walinzi wa pwani ya Italia katika bahari ya Mediterani
Kikosi cha ulinzi wa pwani ya Italia kimesema kimewaokoa zaidi ya wahamiaji elfu mbili wakisafiri katika maboti katika bahari ya Mediterani-- katika operesheni kubwa kuliko zote kufanywa kwa wakati mmoja mpaka sasa.
Meli za jeshi la wanamaji wa Italia na meli za mizigo za kibiashara pia zilizuhiska katika operesheni hiyo.
Kikosi cha walinzi wa pwani kinasema kwa mara ya kwanza walikabiliana na watu wenye silaha wanaofanya biashara ya kusafirisha watu na kuhatarisha maisha ya wafanyakazi wake.
Wengi wa wahamiaji ambao waliondoka kutoka Libya na kujaribu kufika kisiwa cha Lampedusa -- walikuwa vijana kutoka nchi za Afrika. (wiki iliyopita zaidi ya wahamiaji mia tatu wanadhaniwa kufa baharini.).
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago