Mwalimu Oscar Samba: Mahali wanafunzi wa Mkuu Sec School. 22/2/19. KISUDIO LA AKILI KIBIBLIA KATIKA KUKUFANIKISHA KIMAISHA.


Mithali 3:19 Kwa hekima Bwana aliiweka misingi ya nchi; Kwa akili zake akazifanya mbingu imara;
Fahamu: Kukosa Akili, au kushindwa kuitumia Akili, huwa na madhara kadha wa kadha:

1. Kutapanya Mali, au Kushindwa kuthamini chenye thamani; Mithali 11:22 Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe, Kadhalika mwanamke mzuri asiye na akili.
Unampeleka shule, anaanza kuvuta bangi, anajiingiza kwenye ukahaba, na makundi hatarishi, uwe na uhakika ni pete yenye thamani ya dhahabu ila imo kinywani mwa nguruwe, yaani kapewa elimu, ila hana akili ya kuithamini, ataichezea na kuiharibu.

2. Uvivu; Mithali 24:30 Nalipita karibu na shamba la mvivu, Na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili.
31 Kumbe! Lote pia limemea miiba; Uso wake ulifunikwa kwa viwawi; Na ukuta wake wa mawe umebomoka.
32 Ndipo nilipoangalia na kufikiri sana; Naliona, nikapata mafundisho.
33 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi!

Biblia inatuambia kuwa uvivu ni tatizo la kutokutumia akili, kwa hiyo, ukimuona mwanafunzi hasomi, au ni mvivu kujisomea,ni mzito kuamka usiku, uwe na uhakika kuwa huyu anaitwa hana au atumii akili, au anatatizo katika akili yake, ikiwa na mantiki kuwa kazi moja wapo ya akili ni kuachilia msukumo wa uhodari na ufanyaji kazi kwa bidii katika masomo au katika kufanikisha usomaji wa mwanafunzi.

3. Dharau ni Dalili ya Mtu Asiye na Akili;  Mithali 11:12 Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza.
Mwanafunzi asiye sikiliza wazazi wake, asiye sikilizawalimu, vio gozi wake, mwenye majigambo na kudharau wenzake, au kujiona ni mwenye thamani kuliko wengine, huyu kibiblia huitwa ni mwenye shida katika kuzitumia akili zake, maana kitu kimoja wapo ambapo akili imepewa ni ili iweze kutengeneza umoja, nithamu, utii, uadilifu, na mshikamano, ndiposa sisi tu tofauti na wanayma, isimizi wanaosifuwa na Mithali, kwamba ni wenye akili, sifa yao moja ni umoja. Sasa penye dharau hakuna umoja, bali pana kujitenga, na kubagua wengine.
Muhimu: Akili ukizitumia vibaya nazo hutumka:

Ikupe kuepuka kutumia akili zako ili kubuni vitu vitakavyo potosha watu zaidi, vitu vitakvyo zidi kuiangamiza jamii, vitu vitakavyo tumika kama silaha ya dhambi, pia kwa akili zako usizitumie kutongozea, au kushawishi wengine ili uzini nao, maana Mithali sita husema huyu hana akili kabisa, wapo wanafunzi wanaozitumia akili zao vibaya, hili ni tatizo katika vitabu vyetu,nimeweka onyo la kuathibiwa, na andiko nikupalo linasema kuwa huyu hana akili, A hiyo hunui kusema kwamba hana kili katika kumjua Mungu, maana amjuaye Mungu hutamani kumpendezesha Yeye, lakini B yake husema kuwa ana akili katika kutenda mabaya ikiwa na maana kwamba, huzitumia akili zake alizopewa na Mungu vibaya, aidha za kuzaliwa kama kipaji ama kipawa, ama uelewa mkubwa zaidi aliopewa. Nia ya pwenti hii ni kukutaadharisha katika matumizi mabaya ya upeo mkubwa uliopewa na Mungu, Paulo Mtume alipewa na hapo awali aliitumia vibaya, akalitesa kanisa,baadae akaja kugundua siri na kuja kuutumia vizuri zaidi katika kuliimarisha, sasa wewe ujumbe huu sii wa bahati mbaya kwako bali ukusukume katika kuzitumia ili uujenge ufalme wa Mungu, mie natumia zangu kuhubiri injili, kuandika vitabu, na kukupasha jumbe kama hizi, zamani nilianza kuzitumi vibaya kwa kutunga Filamu na Hadhithi, ila sasa nazielekeza msalabani ! Wewe je? Umepewa kuimba, au kupiga ala za Muziki, jiulize unapiga katika Bwana au katika Lusifa! Unaimba nyimbo zakumuimbia Mungu au Shetani? 

Yeremia 4:22 Kwa maana watu wangu ni wapumbavu, hawanijui; ni watoto waliopungukiwa na akili, wala hawana ufahamu; ni wenye akili katika kutenda mabaya, bali katika kutenda mema hawana maarifa.
Utendaji wa Akili:

1. Ndani ya Kipawa au Kipaji Kuna Akili;
Kutoka 35:31 naye amemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na akili, na ujuzi, na kazi ya ustadi kila aina;
:35 Amewajaza watu hao akili za moyoni, ili watumike katika kazi kila aina, ya mwenye kuchora mawe, na kazi ya werevu, na ya mwenye kutia taraza, katika nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri, na ya mwenye kufuma nguo; ya hao wafanyao kazi yo yote, na ya wenye kuvumbua kazi za werevu.

Kwa hiyo, uimbaji ni akili za uimbaji, muandisi, mkemia ama mwanabaolojia ni akili katika alichokisomea,kiongozi ana akili za uongozi, hii ikupe kukaa vyema kwenye karama na kipawa ulichopewa na Mungu, ili utumie kwa utukufu wake.

2. Akili Kidhiirika katika Utendaji Ndipo huweza kukusaidia, ile una akili lakini hauitumi, ni sawa na kuwa na umeme usioutumika, ni sawa na mtu mwenye maji ila hayatumii, kiu haiondoki kwa kuwa na maji, bali kwa kuyanywa, na ufahamu kuwa huwezi kuyanywa kama huna, kwa hiyo kuwa nayo ni muhimu, kisha kuyatumia pia.
Yusufu alikuwa na akili ila yupo jela, alipotoka, akili yaje ikadhiirika, hii ikupe kujiombea ili kujitoa kwenye vifungo vikamatavyo akili, kama kufungwa fahamu na kadhalika.

Kuna wanafunzi waliwekwa jela za kuvuta bangi, jela za uzinifu, jela za kiburi, na kila tabia hatarishi ikiwemo ya kutokutii ama kuheshimu wazazi wao na walimu, huyu ujuwe adui ananuia kuzizuilia akili zake zisiwe na matunda maana hazipo katika utendaji, akiadhibiwa kusimamishwa shule, ama kukosa utulivu wa kujisomea kwa sababu ya hizo tabia, uwe na uhakika,akili yake, haiwezi kukua, maana maarifa ya darasani ndiyo ya kuzayo akili yake!

Tujionee kwa Yusufu; Mwanzo 41:12 Na huko pamoja nasi palikuwa na kijana; Mwebrania, mtumishi wa mkuu wa askari, tukamhadithia, naye akatufasiria ndoto zetu; akamfasiria kila mtu kama ilivyokuwa ndoto yake.

Ni mujiza pekee ndio ulitengeneza mwanya wa akili zake kuanza kuchanua akiwa jela; 

Baada ya kutoka Jela, ndipo matunda ya akili yake hujidhiirisha, kwanza jionee utendaji wake; 
Mwanzo 41:39 Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe.

Matunda: Mwanzo 41:40 Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu, na kwa neno lako watu wangu watatawaliwa. Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe.

3. Hukupa Kujiwekea Akiba ya Maarifa; 
Mithali 10:14 Watu wenye akili huweka akiba ya maarifa; Bali kinywa cha mpumbavu ni uangamivu ulio karibu.
Kwa hiyo,mwanafunzi mwenye akili, hujituma katika kujisomea.
4. 

NB: Akili zinahesabika, au kupimika, kwa hiyo, muombe Mungu akuongezee kama una huo uhitaji:
Lakini kabla ya kuongezewa au kuyaomba hayo, hakikisha ulizo nazo zinatumika vizuri, au unuie kuzitumia vizuri, pili hakikisha unazifungua, au kuzikomboa ulizo nazo, kama kuomba moyo wa ufahamu na kukomboa fikra zako kwa Damu ya Yesu.

1 Wafalme 4:29 Mungu akampa Sulemani hekima, na akili nyingi sana, na moyo mkuu, kama mchanga ulioko pwani.
Mithali 30:24 Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo; Lakini vina akili nyingi sana.

Zekaria 9:2 na Hamathi pia iliyo mpakani mwake; na Tiro, na Sidoni, kwa maana ana akili nyingi.
Zekaria 9:3 Na Tiro alijijengea ngome, akakusanya fedha kama mchanga, dhahabu safi kama matope ya njia kuu.
Fahamu Sana: Asiye na Akii, au Asiyetumia Akili, ama Ambaye akili zake zimefungwa, au kuzuiliwa, huwa mzito kuelewa; 
Mathayo 15:14 Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.
15 Basi Petro akajibu, akamwambia, Tueleze mfano huo.
16 Yesu akasema, Hata sasa ninyi nanyi mngali hamna akili?
17 Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni?
Kwa hiyo, Muombe Mungu azifunuliye akili zako ili zipate na kuelewa; 
Luka 24:45 Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.
46 Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu;
47 na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu.
48 Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya.
BWANA YESU, NIMETAMBUA KUWA MIMI NI MWENYE DHAMBI, NATUBU MBELE ZAKO LEO, NISAMEHE NA NINAKUOMBA UFUTE JINA LANGU KWENYE KITABU CHA HUKUMU, TAFADHALI LIANDDIKE KWENYE KITABU CHA UZIMA, NINAKUKIRII NA KUKUPOKEA MOYONI MWANGU KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, HAKIKA WEWE NI MUNGU NA ULIFUFUKA KATIKA WAFU, Amen.

Hongera kwa kuokoka na tafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo, kwa maombi, sadaka kwa njia ya M-Pesa, kupiga simu au Wasats App, ni +25559859287. Tupo Arusha Tanzania.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company