Makundi mbalimbali yalaani vitisho vya polisi huko Kenya



Makundi mbalimbali ya kiraia pamoja na vyama vya kutetea haki za waandishi wa habari nchini Kenya zimelaani vitisho dhidi ya wanahabari vilivyotolewa na Inspekta Mkuu wa Polisi, David Kimaiyo hapo jana. Chama cha Wanasheria nchini Kenya (LSK) kimesema hatua ya Bw. Kimaiyo inalenga kuirudisha nchi katika zama za utawala wa kiimla ambapo vyombo vya habari havikuwa na uhuru wowote wa
kuwaeleza watu ukweli wa Mambo. Tume ya Kitaifa ya Kutetea Haki za Binadamu (KNCHR) ni taasisi nyingine iliyolaani matamshi ya Insepkta Mkuu wa polisi kuhusu vyombo vya habari na wanahabari kwa ujumla. Kimaiyo amesema vyombo vya habari vinaeneza propaganda kuhusu shambulizi la kigaidi dhidi ya jumba la maduka la Westgate lililotokea majuma kadhaa yaliyopita. Mkuu huyo wa polisi amesema wanahabari wanaotoa taarifa za uchochezi kuhusu tukio hilo watakamatwa na kushtakiwa. Kuna habari kwamba, polisi inawasaka waandishi 2 wa habari wa televisheni ya KTN kwa kuandaa kipindi cha upelelezi ambacho kimewaonyesha wanajeshi wa Kenya wakipora bidhaa wakati wa tukio la Westgate.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company