HI HAPA RASIMU YA KWANZA YA KATIBA YA WANAFUNZI WA CHUO CHA A.J.T.C

CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA








RASIMU YA KATIBA YA WANAFUNZI
2014


YALIYOMO
Ibara    Kichwa cha habari
SURA YA KWANZA
SERIKALI YA WANAFUNZI,BUNGE,SPIKA WA BUNGE,UTAWALA MKUU WA CHUO NA BARAZA LA KATIBA NA SHERIA.
SEHEMU YA KWANZA.
1.VIONGOZI WA WANAFUNZI……………………………………………………………………………………….
2.BUNGE LA WANAFUNZI NA SPIKA WA BUNGE…………………………………………………………………........................................
3.BARAZA LA SHERIA NA KATIBA…………………………………………………………………………………........................
SEHEMU YA PILI
4.UTAWALA MKUU WA CHUO………………………………………………………………………………………….
SEHEMU YA TATU
5.RAIS WA SERIKALI YA WANAFUNZI……………………………………………………………………………………………..
6.MAKAMO WA RAIS WA SERIKALI YA WANAFUNZI………………………………………………………………………
7.AFISA UHUSIANO WA SERIKALI YA WANAFUNZI……………………………………………………….
8.KATIBU WA SERIKALI YA WANAFUNZI………………………………………………………………………
SURA TA PILI.
BARAZA LA MAWAZIRI,HAKI,MLEZI WA WANAFUNZI,ELIMU, HABARI,NIDHAMU,SHERIA NA UTAWALA BORA.
SEHEMU YA KWANZA
9.BARAZA LA MAWAZIRI……………………………………………………………………………………………
10.HAKI ZA WANAFUNZI…………………………………………………………………………………………………
11.MLEZI WA WANAFUNZI…………………………………………………………………………………………….
SEHEMU YA PILI
12.ELIMU………………………………………………………………………………………………………………………..
13.HABARI…………………………………………………………………………………………………………………….
SEHEMU YA TATU.
14.NIDHAMU……………………………………………………………………………………………………………………….
15.SHERIA, KATIBA NA UTAWALA BORA………………………………………………………………………………..
SURA YA TATU.
MICHEZO, BURUDANI,AFYA, MAKAZI.
SURA YA KWANZA
16.MICHEZO NA BURUDANI………………………………………………………………………………………….
17.AFYA NA MAKAZI. ……………………………………………………………………………………………………..
SURA YA NNE.
MAADILI YA WANAFUNZI,VIONGOZI, WALIMU NA WAJIBU.
SEHEMU YA KWANZA
18.MAADILI YA WANAFUNZI………………………………………………………………………………………….
19.MAADILI YA WALIMU KWA WANAFUNZI. …………………………………………………………………………
20.MAADILI KWA VIONGOZI WA WANAFUNZI. ……………………………………………………………………
SEHEMU YA PILI
21.WAJIBU  WA MWANAFUNZI. …………………………………………………………………………………….
22.WAJIBU WA MWALIMU KWA MWANAFUNZI ……………………………………………………………………
SURA YA TANO
ULEZI WA DARASA,UCHAGUZI NA UDHIBITI WA MATUMIZA MABAYA YA FEDHA.
SEHEM YA KWANZA
23. MWALIMU WA DARASA ……………………………………………………………………………………………
24.WAWAKILISHI WA DARASA …………………………………………………………………………………………

SEHEMU YA PILI.
25.TUME HURU YA UCHAGUZI YA WANAFUNZI WA  CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA…..……………………………………………………………………
SEHEMU YA TATU
26.MKAGUZI WA HESABU NA MATUMIZI YA FEDHA ZA VIONGOZI WA WANAFUNZI…………
                                           
UTANGULIZI.
Kwa hiyari yetu sisi wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji  Arusha,tumeamua kuwa na katiba hii ambayo itakuwa ndio msingi mkuu wa sheria na kanuni katika maisha yetu hapa chuoni.
Dhumuni la katiba hii ni kudumisha amani,haki na kutimiza madhumuni na shabaha pamoja na maono yanayotufanya tuwepo hapa chuoni.













SURA YA KWANZA
SERIKALI YA WANAFUNZI,BUNGE,SPIKA WA BUNGE,UTAWALA MKUU WA CHUO NA BARAZA LA KATIBA NA SHERIA.
SEHEMU YA KWANZA.
1.VIONGOZI WA WANAFUNZI.
(1)Kutakuwa na viongozi wa wanafunzi watakao gawanyika katika nguzo kuu tatu,nguzo hizo ni;
(a)   Serikali ya wanafunzi,nguzo hii itakuwa chini ya kiongozi mkuu ambaye ni Rais wa serikali ya wanafunzi,jukumu lake kubwa ni kuwaongoza wanafunzi.
(aa)Viongozi wengine waliopo katika nguzo hii ni; Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi, Katibu wa serikali ya wanafunzi, Afisa uhusiano wa serikali ya wanafunzi, baraza la mawaziri,Idara/kamati za serikali ya wanafunzi kwenye vitengo mbalimbali na Wawakilishi wa darasa.
(b)   Nguzo ya pili ni Bunge,nguzo hii itakuwa chini ya kiongozi mkuu ambaye ni spika wa bunge.Jukumu lake  kubwa ni kutunga sheria na kuisimamia serikali.
(c)    Nguzo ya tatu ni baraza la sheria na katiba,nguzo hii ipo chini ya kiongozi mkuu mwenye cheo cha mwenyekiti kiongozi, jukumu kubwa la baraza hili ni kutafsiri sheria
2.BUNGE LA WANAFUNZI NA SPIKA WA BUNGE.
(1).Kutakuwa na bunge la wanafunzi litakaloongozwa na spika wa bunge.Pia wabunge wake watachaguliwa na wanafunzi kwa utaratibu uliopo kwenye ibara ya 25 (6)
(2).Majukumu ya bunge/mbunge.
(a)               Kuwaondoa viongozi walioshindwa kutekeleza wajibu wao madarakani akiwemo Rais,
(b)               Kutunga sheria,
(c)                Kujadili na kupitisha sera,kanuni na mipango ya serikali ya wanafunzi,
(d)               Kusimamia idara zilizopo chini yeke,
(e)               Kuisimamia na kiushauri serikali ya wanafunzi,
(f)                 Kuidhinisha au kutokuridhia uteuzi wa baadhi ya viongozi,
(g)               Kuikosoa na kufuatilia mwenendo na utendaji wa serikali ya wanafunzi.
(3)Majukumu ya Bunge yanaweza kuongezeka kulingana na kanuni zake.
(4)Bunge litapaswa kutengeneza kanuni ambazo zitaunda muundo mzima wa uongozi wa bunge na jinsi ambavyo litafanya shughuli zake.
(5)Kama bunge litapoteza imani na Raisi,Makamu wa Raisi, Afisa uhusiano  au Katibu wa serikali ya wanafunzi, litalazimika kufuata Utaratibu ufuatao ili kumondoa madarakani;
(a)   Hatua ya kwanza,lazima kuwe na sababu za msingi, sababu hizo zweza kuwa;
(aa)Kushindwa kutekeleza wajibu wake kwa muda wa siku sitini mfululizo kutokana na uzembe,
(bb)Kuugua ugonjwa wa akili,
(cc)Kuugua maradhi yoyote ambayo yanamzuia kutekeleza wajibu wake  kwa muda wa siku sitini mfululizo,
(dd)Kukiuka misingi ya uongozi, sheria na katiba ,maadili ya uongozi na uanafunzi,
(ee)Kufanya kosa kubwa lililosababisha kupewa adhabu ya kusimamishwa masomo kwa zaidi ya kipindi cha muda wa siku thelathini, ila kosa na adhabu hiyo lazima  vithibitishwe na baraza la sheria na katiba ya kwamba ni halali .
(b)   Bunge litajadili sababu husika na kupiga kura ya kutokuwa na imani na kiongozi huyo.
(c)    Kama idadi kubwa ya kura itaonesha kutokuwa na imani na kiongozi huyo,tume ya uchaguzi itapaswa kuchukua hatua ikiwemo kusitisha uchaguzi wa nafasi hiyo kwa kufuata taratibu husika.
(6) Spika wa bunge ndiye atakayekuwa kiongozi mkuu wa shughuli zote za bunge.
3.BARAZA LA SHERIA NA KATIBA.
(1)Kutakuwa na baraza la sheria na katiba.
(2) Baraza hili litagawanyika katika ngazi kuu mbili ambazo ni ngazi ya juu na ngazi ya chini ya maamuzi.
 (3) Muundo wa uongozi wa ngazi ya juu.
(a)   Ngazi hii itakuwa na viongozi wakuu watatu na wajumbe wengine wane.
(b)   Kiongozi mkuu wa ngazi hii atakuwa na cheo cha Mwenyekiti kiongozi.
(c)    Msaidizi wake  atakuwa ni makamu mwenyekiti.
(d)    Pia kiongozi mwingine atakuwa ni katibu wa baraza hili.
(e)   Wajumbe hao wanne watachaguliwa na viongozi hawa watatu kwa sifa na vigezo vitakavyowekwa na bunge.
(f)     Viongozi hawa wakuu watatu watachaguliwa na bunge kwa sifa na vigezo watakavyoviweka  ambavyo lazima vihusishe  uwezo na upeo wao wa kisheria pamoja na uadilifu wao.
(g)   Wanapaswa kuhakikisha ngazi ya chini inatimiza wajibu wake au wao au kuutekeleza kutokana na sababu mbalimbali pale wanaposhindwa kufanya hivyo.
(h)   Pia wanapaswa kupitia maamuzi yote ya kiutendaji yanayofanywa na ngazi ya chini.
(i)     Bila kuathiri masharti yoyote ya katiba hii na sheria nyinginezo , viongozi hawa hawatawajibika kwa bunge wala kuondolewa madarakani  na bunge ila kama wanafunzi watakosa imani na kiongozi au baraza zima watapaswa kupiga kura ya kutokuwa na imani aidha na baraa zima au kiongozi husika.Kura hiyo itasimamiwa na tume huru ya uchaguzi  ya wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji  Arusha .
 (4) Majukumu ya ngazi ya juu.
(a)   Ngazi ya juu itahusika na rufaa kutoka ngazi ya chini Ufafanuzi wa kisheria pamoja na hukumu.
(b)   Wanapaswa kusikiliza kesi zenye kuhitaji maamuzi makubwa ikiwemo;
 (aa) Utata katika hukumu au maamuzi ya Kufukuzwa chuo kwa mwanafunzi
(bb)Kusimamishwa masomo kwa mwanafunzi au adhabu ya wiki mbili mfululizo,
(cc)Maamuzi ya Bunge yenye utata, serikali au utawala wa juu wa chuo.
(5)Viongozi wa ngazi hii ndio watakokuwa viongozi wakuu wa baraza hili.
(6)  Kwa utashi au kulingana na ukubwa wa tatizo ngazi ya chini inaweza kupeleka shauri au tatizo                               lolote kwenye ngazi hii ya juu ambapo bila kujadili uamuzi huu,ngazi hii itapaswa kulifanyia kazi.
(7) Ngazi hii ya chini ya maamuzi itahusisha viongozi watakaoteuliwa na Rais na kupitishwa na baraza la mawaziri.-
(a)   Viongozi hawa watakuwa watatu na wataitwa wanadhimu,kiongozi wao ataitwa mnadhimu mkuu.
(b)   Ngazi hii itahusika na ufafanuzi wa sheria na utafsri wa sheria, pia makosa madogo yenye kuhitaji adhabu ndogo.
(c)    Ngazi hii inapaswa kuhakikisha ya kwamba serikali inatunga kanuni kwa kupitia wizara zake, ambazo zitakuwa za haki,na zenye kukidhi mahitajio.
(8) Maamuzi yoyote yatakayochukuliwa na baraza hili la sheria na katiba lazima yahusishe usikilizwaji wa pande zote mbili yaani mlalamikiwa na mlalamikaji.
(9) Ngazi ya juu ya baraza hili halitakuwa na uhalali wa kutoa maamuzi bila kuwa na kikao rasmi kitakachohusisha wajumbe zaidi ya wawili na viongozi wawili kati au wote watatu wakuu.
 (10) Ngazi ya chini inaweza kutoa maamuzi bia kikao na maamuzi hayo yanaweza kufanywa na mnadhimu mmoja bila kumshirikisha mwingine kama kuna sababu ya msingi.
 (11) Maamuzi yote yatakayokuchuliwa na ngazi ya juu ya baraza hili lazima yawe ni kwa mujibu wa katiba hii,sheria au kanuni halali.Pia ngazi ya chini ya maamuzi itapaswa kutoa  maamuzi kwa vigezo hivyo ila hekima,desturi na busara zinaweza kutumika katika maamuzi yao lakini katika kutoa adhabu ndogo na sio katika kuongeza adhabu.Kipengele hiki hakiwapi mamlaka viongozi wa ngazi ya chini kuvunja kipengele chochote cha katiba hii,sheria kanuni wala taratibu zozote zile halali.
(12)Kama mtuhumiwa hataridhika na maamuzi kutoka kwenye ngazi ya juu ya baraza hili anapaswa kupeleka malalamiko yake kwa mlezi wa wanafunzi ambaye atapaswa kuyapitia na akiona yana mantiki atakutana na baraza la sheria na katiba ili shauri hilo lipitiwe upya.
(13)Kabla ya kutoa hukumu wajumbe watakutana na kukubaliana katika maamuzi,kama wajumbe watatofautiana maamuzi watapaswa kukaa kwa pamoja wajumbe wanaokubalina kimaamuzi na kuandaa hukumu.Mara baada ya hatua hiyo kila pande itasomo maamuzi yao mbele ya mlalamikaji na mlalamikiwa na upande utakaoungwa mkono na wajumbe wengi kwa kura mbele ya mlalamikaji na mlalamikiwa ndio utakaoshinda.
SEHEMU YA PILI
4.UTAWALA MKUU WA CHUO.
(1).Katiba hii inatambua uwepo wa utawala mkuu wa chuo ambao kiongozi wake mkuu ni mkurugenzi wa mafunzo wa chuo hiki cha Uandishi wa Habari na Utangazaji  Arusha.Pia unahusisha wakufunzi wote wa chuo hiki pamoja na idara zake.
(a)   Utawala huu unafanya kazi kwa mujibu wa katiba waliyonayo na katiba hii ya wanafunzi.
(2)Ufuatao ni wajibu wake kwa wanafunzi;
a)      Kuheshimu,kutii na kuilinda katiba hii ya wanafunzi wa cho cha Uandishi wa Habari na Utangazaji  Arusha,pia sheria,kanuni na taratibu halali zilizowekwa na wanafunzi, serikali ya wanafunzi,bunge au baraza la sheria na  katiba.
b)      Unawajibu wa kufuatilia mwenendo wa wanafunzi na vyombo vyao vyote vya uongozi.
c)      Unapaswa kuhakikisha unatimiza malengo na dhamira ya wanafunzi kuwepo chuoni hapa na kutoa haki zao za msingi kama ilivyo kwenye mitaala,taratibu za NACTE au wizara yenye dhamana husika ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,katiba,sheria au taratibu pia kama ilivyoainishwa kwenye fomu ya kujiunga na chuo.
d)      Hautakuwa na mamlaka yoyote ile ya kuivunja serikali ya wanafunzi,bunge, baraza la sheria na  katiba wala kushinikiza kujiuzulu au Kusimamishwa madaraka  kwa kiongozi yeyote wa wanafunzi bila kufuata Utaratibu uliopo kwenye 4(3).
(3) Kama kiongozi yeyote wa utawala wa juu wa chuo ,serikali ya wanafunzi au mwanafunzi yeyote au darasa litapoteza imani na kiongozi  yeyote wa ngazi yoyote wa wanafunzi aidha kweye serikali,bunge au baraza la katiba; hanabudi kufuata utaratibu ufuatao:
(a)Watapaswa kupeleka malalmiko yao kwa Afisa uhusiano wa serikali ya wanafunzi au mlezi wa serikali ya wanafunzi.
(b)   Mlezi wa wanafunzi au Afisa uhusiano  wa wanafunzi wakiyaona malalamiko hayo ni ya msingi watapaswa kuyapeleka kwenye ngazi zifuatazo;
(aa)Kama malalamiko hayo yanamhusu  waziri au baraza lake, watapaswa kuyapeleka kwa Rais wa wanafunzi ili achukue maamuzi stahiki mara baada ya kuyatafakari kwa kina.
(bb)  Kama malalamiko hayo yatamhusu kiongozi yeyote wa idara au kamati yoyote ile basi watayapeleka kwenye wizara yenye dhamana husika ili wizara hiyo ichukue maamuzi stahiki,
(cc)Kama malalamiko hayo yanamhusu Kiongozi wa idrara ya ukaguzi wa  hesabu za fedha na matumizi ya wanafunzi,au mbunge,Afisa uhusiano,Makamu wa Rais,Katibu wa wanafunzi au Spika wa bunge.
 (dd)Kama malalamiko hayo yanalihusu Bunge, basi malalamiko hayo yatapelekwa kwa spika wa bunge , bunge litayajadili na kuyachukulia hatua stahiki.
(ee)Kama malalamiko hayo yatamhusu kiongozi wa darasa,basi Afisa uhusiano  au mlezi wa wanafunzi atapaswa kushirikiana na wizara ya elimu na kuyafikisha kwa darasa husika ili wachukue maamuzi stahiki.
(ff)Kama malalmiko hayo yatamhusu Raisi basi yatapaswa kupelekwa kwa spika wa bunge na bunge litafuata Utaratibu uliowekwa kwenye ibara 2 (5)
SEHEMU YA TATU
5.RAIS WA SERIKALI YA WANAFUNZI.
(1).Kutakuwa na Rais wa serekali ya  wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji  Arusha, atakayechaguliwa na wanafunzi kwa mujibu wa matakwa ya katiba hii ya chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji  Arusha
(2).Rais ndyie kiongozi mkuu wa ngazi zote kwa serikali ya wanafunzi.
(3).Yafuatayo ni majukumu ya Rais.
(a)   Kuteua baraza la mawaziri na pia kulivunja punde litakapokiuka misingi na taratibu zautendaji kazi.
(b)    Kuvunja Bunge la wanafunzi siku kumi na tano kabla ya kuanza zoezi la uchaguzi mkuu au punde litakapokiuka misingi yake ya utawala
(c)    Ni mshauri wa wanafunzi na walimu dhidi ya wanafunzi.
(d)   Kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa wajibu wa wanafunzi na utimizwaji wa haki zao.
(e)   Anapaswa kutekeleza wajibu wake kama mwenyekiti katika vikao vyote vya baraza la mawaziri, vikao vingine muhimu  na baraza la wanafunzi.
(f)     Ndiye mwenye maamuzi ya mwisho katika serikali ya wanafunzi.
6.MAKAMU WA RAIS WA SERIKLI YA WANAFUNZI.
(1).Kutakuwa na makamu  wa Rais; atahitajika kupendekezwa na Rais na kugombea nae kama mgombea mwenza wakati wa uchaguzi, na punde atakapoondoka madarakani Rais atamteua makamu mwingine.
(2)Majukumu yake;
a)      Ndiye mshauri na  msaidizi mkuu wa Rais,
b)      Atapaswa kutekeleza majukumu na kuchukua mamlaka ya Rais wakati Rais akiwa nje ya ofisi.
c)      Atapaswa kukaimu nafasi ya Urais endapo Rais;     
                    (aa).Atafariki, 
                    (bb).Atajiuzulu
(cc).Ataugua mfululizo kwa zaidi ya miezi miwili.
(dd).au Ataondolewa na Bunge.   
(cc)Kusimamishwa masomo.
(3)Makamu wa Rais atakaimu nafasi hiyo kwa kipindi chote ambacho tume itakuwa ikiandaa utaratibu wa uchaguzi mdogo au mkuu kwa ajili ya nafasi hiyo. Kipindi hiki hakitapaswa kuzidi siku kumi na nne.
(d) Atapaswa kuwa mjumbe kwenye kikao cha baraza la mawaziri.
(e) Atashirikiana na Rais kiushauri katika uteuzi na muundo wa baraza la mawaziri.
(f) Atapaswa kusikiliza na kutekeleza shughuli zote atakazoagizwa na Rais.
(4) Bila kuathiri masharti yoyote ya katiba hii makamu wa Rais hatakuwa na uwezo wa kuchukua majukumu mazito ya Rais wakati Rais akiwa nje ya ofisi kwa kipindi chochote bila kupata kibali cha Rais .Majukumu hayo yaweza kuwa;
a)      Kulivunja baraza la mawaziri au ,
b)       Kulivunja Bunge

7.AFISA UHUSIANO WA SERIKALI YA WANAFUNZI
(1).Kutakuwa na afisa uhusiano wa wanafunzi, atachaguliwa na wanafunzi kupitia utaratibu uliowekwa na tume huru ya uchaguzi ya wanafunzi wa  wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji  Arusha
(2).Majukumu yake.
a)      Ndiye msemaji mkuu wa wanafunzi na serikali yao.
b)      Anajukumu la kudumisha au kutengeneza mahusiano mazuri kati ya walimu na wanafunzi,
c)       Anapaswa kutetea haki,maslahi ya wanafunzi na kufuatilia uwajibikaji wa  wanafunzi pia walimu dhidi ya wanafunzi.
d)       Atapaswa kuhudhuria vikao vya baraza la mawaziri kama mjumbe.
e)      Atafanya kazi kwa kushirikiana na mlezi wa wanafunzi.
f)       Anapaswa kusikiliza malalamiko,ushauri kutoka kwa wanafunzi au walimu dhidi ya wanafunzi na kuyatatua/kuyafanyia kazi au kuyafikisha sehemu husika.
g)      Atakuwa na jukumu la kutengeneza na kujenga taswira safi dhidi ya wanafunzi/chuo pia atakuwa na jukumu la kusafisha taswira ya wanafunzi au serikali  yao.

8.KATIBU WA SERIKALI YA WANAFUNZI.
(1).Kutakuwa na katibu wa serikali ya wanafunzi, atakayechaguliwa na wanafunzi kupitia utaratibu uliowekwa na tume huru ya uchaguzi ya wanafunzi wa  chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji  Arusha.
(2).Yafuatayo ni majukumu yake;
a)      Katibu huyu ndiye atakayekuwa mratibu wa shughuli zote za kila siku za serikali ya wanafunzi.
b)      Atapaswa kupeleka ripoti zote,shughuli na maazimio ya Bunge la wanafunzi na baraza la mawaziri pia uwajibikaji, na ufanisi wa kila wizara au waziri mmoja mmoja  kwa Rais wa serikali ya wanafunzi.
c)      Atakuwa msimamizi wa shughuli zote za kiserikali bungeni ambapo atashiriki kama waziri.
d)      Atapaswa kumshauri Rais kuhusu utendaji na uwajibikaji  wa waziri/wizara au kiongozi yeyote aliepo katika nguzo ya serikali.
e)      Atapaswa kutekeleza majukumu na shughuli atakazoagizwa na Rais au makamu wake.
f)       Atapaswa kuandaa vikao vyote vya baraza la mawaziri au vikao vingine halali na kuhifadhi kumbukumbu ya maazimio au maudhui ya vikao hivyo,
g)      Ndiye msimamizi wa vikao hivyokiratiba na kiajenda ,
h)      Bila kuathiri mashariti yeyote ya katiba hii, katibu hataingilia majukumu ya Rais kwenye vikao hivyo; Kwani Rais  ndiye mwenyekiti  na msemaji mkuu wa vikao hivyo.

SURA TA PILI.
BARAZA LA MAWAZIRI,HAKI,MLEZI WA WANAFUNZI,ELIMU, HABARI,NIDHAMU,SHERIA NA UTAWALA BORA.
SEHEMU YA KWANZA
9.BARAZA LA MAWAZIRI.
(1).Kutakuwa na baraza la mawaziri litakaloteuliwa na Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha.
(2).Sifa za mawaziri.
(a)   Achaguliwe  kutokana na uwezo alionao kwenye wizara husika.
(b)   Awe na uwezo wa kuyamudu majukumu ya wizara husika.
(c)    Aridhie nafasi hiyo.
(d)   Asiwe na wadhifa wowote baada ya kuchaguliwa kwenye  serikali ya wanafunzi,bunge, baraza la sheria na katiba wala tume ya uchaguzi ya wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji  Arusha.
(3).Majukumu ya mawaziri.
(a)   Kusimamia idara/kamati  zote zilizopo chini yao.
(b)   Mawaziri/waziri anapaswa kutekeleza wajibu na shughuli zake zote kama alivyoagizwa na  Raisi,makamu wa Rais au katibu pia kwa mujibu wa kanuni,taratibu,sheria au katiba zote mbili yaani ya utawala wa juu wa chuo au katiba hii ya wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji  Arusha.
(c)    Kutengeneza kanuni au sera za serikali kwa kupitia utaratibu utakaopangwa na bunge.
(d)   Mawaziri watapaswa kuiwakilisha serikali bungeni kwa kupitia majukumu yao ya kiwizara
    (aa)Mawaziri wakiwa bungeni hawatahesabika kama wabunge na hawatakuwa na haki yoyote ya kibunge badala yake watahitajika kutolea maswala ufafanuzi baada ya kupata kibali kutoka kwa spika wa bunge.
      (bb) Mawaziri hawa wakiwa bungeni wataketi sehemu tofauti na wabunge pamoja na katibu wa serikali ya wanafunzi.
      (cc)Waziri akihitaji kutolea swala ufafanuzi kwa utashi wake pasipo kuhitajika kufanya hivyo na wabunge kupitia spika wa bunge, atapaswa kupeleka ombi kwa katibu wa serikali ya wanafunzi atakayepaswa kulipeleka kwa spika wa bunge ambaye ndiye mwenye wajibu wakutoa kibali.
(4).Adhabu itatolewa kwa waziri au kiongozi mwingine yeyote atakayetoa siri halali ya baraza la mawaziri,serikali au kikao chochote halali; Adhabu hizo zaweza kuwa,
(a)    Kusimamishwa uongozi,
(b)   Kufukuzwa uongozi au
(c)    Adhabu yoyote halali na stahiki.

10.HAKI ZA WANAFUNZI.
(1).Kila mwanafunzi anayo haki ya kuthaminiwa kwa imani yake ya kidini.
(2).Ni haki ya wanafunzi kupata majibu na ufafanuzi wa maoni yao au maswali  yaliyopo kwenye sanduku la maoni kwenye baraza la chuo.
(3).Sanduku la maoni litapaswa kukaa kwenye mazingira rafiki kwa wanafunzi.
(4).Ni haki ya mwanafunzi kusikilizwa,uhuru wa kutoa maoni yake na kupata majibu sahihi kutoka kwenye mamlaka husika.
(5).Ni haki ya mwanafunzi kupata muongozo wa ratiba kuhusu mambo yote muhimu kwa muda watakaokuwepo chuoni kutoka kwa mamlaka husika.
(6). Ni haki ya mwanafunzi kupata ruhusa ya kuahirisha masomo yake kwa muda pale atakapokuwa na sababu au tatizo la msingi,yaweza kuwa;
(a)   Ujauzito  (b) Ajali (c) Ukosefu wa ada/fedha (d) Maradhi  (e) Au sababu zozote zenye uzito mkubwa.
(7). Mwanafunzi atakayerejea ataendelea na muhula aliouwacha pia hakutakuwa na malipo ya ziada kama hapo awali alishalipia muhula huo.
(8).Ni haki ya mwanafunzi kusoma/kufundishwa masomo yote kama ilivyo kwenye Utaratibu wa chuo au mtaala.
(9). Ni haki ya mwanafunzi kupata vifaa kutoka kwenye mamlaka husika kwa ajili ya elimu ya vitendo.
(10).Bila kuadhiri kipengele chochote cha katiba hii au ya utawala wa juu wa chuo  wala kanuni yoyote au sheria, mwanafunzi atakefanya kosa nje ya eneo la chuo na ikabainika hakulifanya kama mwanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji  Arusha  na wala hakuwa kwenye masomo ya vitendo; mwanafunzi huyo hatahukumiwa kama mwanafunzi wa chuo.

11.MLEZI WA WANAFUNZI.
(1)Kutakuwa na mlezi wa wanafunzi atakayeteuliwa na utawala mkuu wa chuo.
 (2)Kama wanafunzi watapoteza imani naye, basi watapaswa kupeleka malalamiko yao kwa katibu wa serikali ya wanafunzi atakayepaswa kuyapeleka kwa  spika wa bunge ili bunge lijadili na kisha kupiga kura ya kutokuwa au kuwa na imani naye.
a)      Kama bunge litakosa imani naye basi katibu wa serikali ya wanafunzi atapaswa kufikishiwa taarifa hiyo kwa utawala mkuu wa chuo ili wachukue hatua stahiki.Utawala huu unaweza kufuta uteuzi wake na kumteua mwingine au kubariki uteuzi wake hali itakayo mfanya aendele na wadhifa huo.
(3) Zifuatazo ni sifa za mlezi wa wanafunzi.
(a)   Awe ni mwalimu katika chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha.
(b)   Awe na uelewa wa kutosha kuhusu wanafunzi.
(c)    Awe amefundisha katika chuo hiki zaidi ya siku sitini.
(d)   Pia awe tayari kuifanya kazi hii.
(4) Majukumu ya Mlezi wa serikali ya wanafunzi;
(a)   Anawajibika kama mshauri na mlezi mkuu wa wanafunzi,serikali ya wanafunzi, bunge na baraza la sheria na katiba.
(b)   Atapaswa kusikiliza na kutatua matatizo yote ya wanafunzi kabla ya kwenda katika ngazi ya juu ya utawala.
(c)    Atapaswa kuhakiki maamuzi yote yaliyofanywa na ,serikali ya wanafunzi,bunge pia baraza la sheria na katiba na kutoa ushauri pale inapobidi,
(d)   Anaweza kufanya vikao na viongozi wa bunge,serikali ya wanafunzi,baraza la sheria na katiba au wanafunzi kadiri aonavyo,
(e)   Kwa kushirikiana na katibu wa wanafunzi na Raisi wa serikali ya wanafunzi, anaweza kuandaa na kushirikishwa kama mjumbe katika kikao cha baraza la mawaziri na kujadili ajenda au kutoa maamuzi na mazimio mbalimbali.
(f)     Anaweza kutoa adhabu kwa mwanafunzi aliyeonesha utovu wa nidhamu kwa kushirikiana na viongozi wa ngazi ya chini ya baraza la sheria na katiba.
(g)   Anapaswa kuhakikisha ya kwamba wanafunzi wote wanaishi katika mazingira safi na salama kiulinzi na kiafya.
(5)Bila kuathiri mamlaka ya katiba hii yaliyopo kwenye ibara hii,kutakuwepo na mlezi wa wanafunzi mwingine atakayejulikana kwa cheo cha mlezi wa maswala ya kijinsia.
(a)   Kama mlezi wa wanafunzi ni jinsia ya kike basi mlezi huyu atakuwa ni wakiume na kama mlezi wa wanafunzi ni jinsia ya kiume basi mlezi huyu atakuwa ni wakike.
(b)   Mlezi huyu atachaguliwa na utawala mkuu wa chuo.
(c)    Mlezi huyu atapokea na kushauri maswala ya kijinsia ambayo mtoaji au mlalamikaji anaona sio busara kuyapeleka kwa mlezi wa waanafuzi ambaye ni wa jinsia tofauti kulingana na maudhui ya maswala husika.
(d)   Mlezi wa jinsia hataruhusiwa kutoa maamuzi yatakayo sababisha kutolewa kwa adhabu bila kupata kibali kutoka kwa mlezi wa wanafunzi ila maamuzi ya upatanishaji au ushauri yapo chini yake.
SEHEMU YA PILI
12.ELIMU.
(1).Mwalimu ambaye hatakidhi mahitaji ya somo; wanafunzi husika watapaswa kufikisha malalamiko yao kwa wizara ya elimu ambayo itakuwa na jukumu la kupeleka kwenye idara ya taaluma ya utawala wa juu wa chuo.
(a) Idara hiyo itapaswa kuyajadili na kuyafanyia kazi ikiwemo kumbadilisha mwalimu mlalamikiwa.
(2).Walimu watakaojiriwa na utawala wa juu wa chuo wanapaswa kukidhi vigezo vya mamlaka husika zinazosimamamia elimu hapa nchini Tanzania ikiwemo Baraza la Taifa la Elimu na Ufundi (NACTE).
(3). Gharama za majaribio, ripoti na mitihani ziainiswe kwenye fomu ya kujiunga na chuo.
(4).Wizara ya elimu itapaswa kutekeleza wajibu na majukumu yake yote ikiwemo;
(a)   Kuhakikisha wanafunzi wanafundishwa masomo yote na kwa kiwango au ubora stahiki.
(b)   Kufanya kazi kwa karibu na Wawakilishi wa dadarasa ili kuchukuwa kero,mapendekezo au maoni ya kitaaluma na kuyafanyia kazi.
(c)    Kutengeneza sera na mipango mbalimbali itakayolenga kuboresha kiwango cha taaluma chuoni.
(d)   Ndio waratibu na wasimamizi wa midahalo au mijadala ya kitaaluma chuoni.

13.HABARI.
(1). Idara zote za habari zitakuwa chini ya wizara ya habari. Kutakuwa na idara kuu tatu,Idara hizo ni;
(a) Idara ya redio.
(b) Idara ya runinga (tv) na,
(c) Idara ya magazeti.
(2). Wizara ya habari itapaswa kutoa matangazo yatakayolenga kuwapata viongozi wa idara hizo kuu tatu kwa muda wa wiki moja.
(a)   Mara baada ya zoezi hilo kukamilika wizara itawafanyia usahili wote waliomba nafasi hizo na kuteua waliofuzu.
(3). Viongozi wa idara hizo hawataruhusiwa kuvifungua, kuvitengeneza, kuvifanyia marekebisho yeyote au kuvipeleka kwa fundi au kwa kiongozi yeyote au mwalimu bila ridha ya mwalimu mwenye dhamana husika.
(4). Mwalimu wa idara husika atapaswa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wizara na viongozi wa idara husika.  
(5). Wizara ya habari pia itapaswa kuhakikisha ya kwamba idara zote zilizopo chini yake inazipangia majukumu na kutimiza.



SEHEMU YA TATU.
14.NIDHAMU.
(1).Mwanafunzi yeyote atakayeshindwa kutekeleza wajibu wake,jukumu au kuonesha utovu wa nidhamu, atapaswa kupewa adhabu.
(2).Adhabu hizo zitatolewa na mwalimu wa chuo hiki au, Baraza la sheria na katiba.
(3).Kiongozi yeyote wa serikali ya wanafunzi Hatokuwa na mamlaka ya kutoa adhabu baada ya kupata kibali cha kufanya hivyo kutoka kwa baraza la katiba na sheria kwa ngazi ya juu au wizara ya nidhamu au sheria na katiba.
(4). Adhabu yoyote itakayotolewa isiwe ya kudhalilisha utu wa mwanafunzi,heshima yake,jinsia au kwenda kinyume na haki za kibinadamu, ikiwemo kuchapwa fimbo, kupigwa makofi au ngumi au kubeba vitu vizito.
 (a) Msingi wa utoaji wa adhabu utapaswa kuzingatia adhabu zile zenye  kulenga kumjenga mwanafunzi kitaaluma ikiwemo kufanya mazoezi ya kimasomo zaidi.
(5). Bila kuathiri masharti yoyote ya katiba hii adhabu itakayotolewa ni lazima iendane na uzito wa kosa kama ilivyoainishwa kwenye, kanuni,sheria au katiba zote mbili yaani katiba ya utawala wa juu wa chuo au katiba hii ya wanafunzi wachuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha.
 (4). Ni kosa mtu ambaye hana hatia kupewa adhabu au kuchukuliwa kama mwalifu .
(a)Haitaruhusiwa kutolewa adhabu kwa kikundi cha watu kwa kosa lilofanywa na mtu mmoja.
(5). Adhabu itatolewa kwa mwanafunzi atakeyebainika kutoa mimba, kumuwezesha kwa kukusudia aidha kiushauri au kifedha mwanafunzi mwingine kutoa mimba; adhabu hiyo yaweza kuwa;
(a)   Kusimamishwa masomo ,
(b)   Kufukuzwa chuo,
 (6).Bila kuadhiri masharti yoyote ya ibara hii yaliyopo kwenye ibara ndogo ya (8), mtuhumiwa hata adhibiwa au kuchukuliwa kama mhalifu hadi uthibitisho wa kitabibu kutoka kwa dakitari wa hosipitali inayotambulika kisheria kuhusu tuhuma hiyo uoneshe kosa hilo na udhibitisho huo uwe na sahihi ya mganga mkuu wa hosipitali hiyo.
(a)   Pili, uthibitisho huo uoneshe dhamira ya mauwaji au ubainishe ya kwamba hakufanya hivyo kutokana na sababu halali za kitabibu zinazotambulika na wizara ya afya ya serikali ya Tanzania.
(7).Mwanafunzi atakayechelewa  kuingia darasani kabla ya robo saa baada ya kipindi kuanza ataruhusiwa kuingia darasani, ila atakaechelewa baada ya robo saa kipindi kuanza hatoruhusiwa kuingia darasani labda kwa sababu maalumu au kibali cha mwalimu wa somo husika.
(a) Pia mwanafunzi huyo hatoruhusiwa kuudhuria vipindi vinavyofuata mara baada ya kipindi husika kumalizika.
15.SHERIA, KATIBA NA UTAWALA BORA.
(1).Katika hali yoyote serikali ya wanafunzi haitavunjwa, bali utaratibu ufuatao utakutumika kama viongozi wake watakiuka misingi ya uongozi hali itakayopelekea  kukosa imani kwa wanafunzi pia walimu.
(a) Mlalamikaji/walalamikaji wawe ni wanafunzi au walimu ambapo watapaswa kupeleka malalamiko yao kwa spika wa bunge au mbunge yeyote ili afikishe kwenye kikao cha bunge.
(b) Mara baada ya bunge kupokea taarifa hiyo litafuata utaratibu wa kumuondoa kiongozi huyo kama ilivyoelekezwa kwenye kanuni zao na katika hii au sheria nyinginezo.
(2).Adhabu kutoka kwenye utawala wa juu wa chuo zitaruhusiwa mara baada ya uongozi wa ngazi ya juu wa serikali ya wanafunzi kushirikiswa na kama uongozi huo utabaini utata au udhaifu kwenye adhabu hiyo unaweza kutoa ushauri kwa utawala huo au kupeleka kwenye baraza la sheria na katiba kwa ajili ya ufafanuzi wa kisheria ; adhabu hizo zaweza kuwa: Kufukuzwa chuo kwa mwanafunzi,
(a)   Kusimamishwa masomo au
(b)   Au adhabu itakayopaswa kufanyika kwa zaidi ya muda wa wiki mbili.
(3).Utaratibu wa bunge kutunga sheria,
(a)   Mbunge,spika wa bunge au katibu wa serikali ya wananfunzi anaweza kupeleka bungeni mapendekezo ya mabadiliko ya sheria au undwaji wa sheria mpya.
(b)   Mara baada ya hatua hiyo bunge litapaswa kuikubali hoja hiyo kwa wingi wa idadi ya kura za wabunge.
(c)    Baada ya hoja hiyo kukubaliwa bunge litajadili mapendekezo hayo.
(d)   Bunge litakaa kama kamati na kupitisha kifungu kimoja baada ya kingine cha mapendekezo hayo.
(e)   Mapendezo hayo yakishaapitishwa yataitwa mswada ambao utasubiri sahihi ya Rais ,Rais atalazimika kuchukua maamuzi kwa siku zisizo zidi kumi na nne mara baada ya kupitishwa na bunge.
(f)      Rais akisaini mswaada huwo utakuwa sheria na kuanza kutumika rasimi mara baada ya kutangazwa kwa wanafunzi wote.
(4)Kama Rais hatatia sahihi, bunge litalizimika kufanya yafuatayo;
(a)   Kujadili mapendekezo au udhaifu ulioainishwa na Rais na kisha kuupitisha upya,
(b)   Au kuupuza na kutokuujadili tena yaani kuachana nao.
(5). Utaratibu wa kubadilisha katiba,
(a)   Bunge litapaswa kuridhia zoezi hili kwa idadi nyingi ya kura,
(b)   Mara baada ya kipengele hicho spika wa bunge ataunda kamati ndogo itakayokuwa na wabunge wa tano, wawakilishi watatu wa madarasa pia Rais na mwenyekiti mkuu wa baraza la sheria na katiba watakuwa ni miongoni mwa wajumbe wa kamati hii.Kazi kubwa ya hii kamati ni kuunda tume ya katiba itakayokuwa na wajumbe wasiopungua kumi wala kuzidi ishirini.
(c)    Tume hiyo itapaswa kukusanya maoni kutoka kwa wanafunzi wa chuo hiki.
(d)   Kuyajadili maoni na kutengeneza rasimu ya kwanza ya katiba.
(e)   Rasimu hiyo ya kwanza itarejeshwa kwa wanafunzi ili ijadiliwe.
(f)     Baada ya hapo  tumeitajadili maoni hayo ya marekebisho na kuunda rasimu ya pili.
(g)   Tume itaunda bunge maalumu la katiba litakalokuwa na wajumbe wawili wawili kutoka kila darasa na wajumbe wote watume ya katiba.Bunge hili litajadili rasimu yote na kupendekeza mapendekezo yake.
(h)    Mara baada ya mapendekezo tume ya katiba itakaa na kuyajadili mapendekezo hayo,kisha kuyapeleka tena kwenye bunge hili maalumu la katiba.
(i)     Bunge maalumu la katiba litapitia hayomarekebisho ya tume na kisha kujiridhisha kwa kupiga kura,ili hatua hii ifanikiwe wajumbe zaidi ya theluthi mbili watapaswa kuiridhia rasimu hiyo.
(j)     Baada ya rasimu hiyo kupita itaitwa rasimu ya pili ambayo itapelekwa kwa wanafunzi kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni ya ndio au laa.
(k)    Rasimu ya pili ikipitishwa na wanafunzi itapelekwa kwa Raisi na mkurugenzi wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazji Arusha kwa ajili ya kupata saini zao.
(l)     Mara baada ya sahihi zao Afisa Uhusiano wa wanafunzi au waziri wa habari atapaswa kutangaza kwa wanafunzi na hapo ndipo itakapoanza kutumika rasimi.
(6)Kama mchakato huu wa katiba utakwama katika hatua yoyote ile basi tume italazimika kufanyia kazi sababu za msingi zilizoikwamisha, ila sabau hizo lazima ziwe na nia na dhamira njema.Pia kama mchakato huwo utakwama kwenye hatua ya kura za maoni ya wanafunzi basi tume inaweza kuanza upya mchakato huo.Ila kama hatua moja itarudiwa kwa zaidi ya mara mbili, bunge la wanafunzi kwa kushirikiana na Raisi laweza kuivunja tume na kuunda nyingine.


SURA YA TATU.
MICHEZO, BURUDANI,AFYA, NA MAKAZI.
SURA YA KWANZA
16.MICHEZO NA BURUDANI.
(1).Ununuzi wa vifaa vyote vya michezo au burudani pamoja na shughuli zote andamizi ikiwemo,uzinduzi wa vifaa/zana hizo,au uifadhi utapaswa kufanyika chini ya wizara husika.
(2).Wizara husika ikishirikiana na mwalimu husika pamoja na kamati/idara husika  itakuwa na dhamana ya kuandaa na kuratibu michezo,matamasha,ligi,bonanza na mashindano mbalimbali aidha ya ndani au nje ya michezo.
(3). Uteuzi wa kamati/idara za michezo/burudani na viongozi wote wa timu za chuo utakuwa chini ya wizara husika.
(4).Kamati/idara zote za michezo/burudani zitawajibika  kwa wizara husika .
 (5). Wizara inayohusika na Michezo/burudani wakishirikiana na mwalimu husika kwenye wizara yao watapanga utaratibu wa kuwapata viongozi wa kamati/idara zao na majukumu yake.
(6).Usajili wa vilabu au timu binafisi na vikundi mbalimbali vya michezo au burudani utakuwa chini ya wizara husika kwa utaratibu watakaouweka; mara baada ya usajili taarifa zitapaswa kwenda kwa mwalimu wa michezo au burudani na pia kwa mlezi wa wanafunzi.
(7). Mwalimu wa michezo/burudani, mwalimu yeyote au kiongozi yeyote wa wanafunzi hawatakuwa na jukumu la kumkataa kiongozi au mjumbe yeyote wa kamati/idara ya michezo au muundo au uwepo wa idara/kamati husika, bali jukumu hilo lipo chini ya wizara yenye dhamana husika.
(8).Kama mwalimu au kiongozi yeyote hataridhishwa na uteuzi au muundo pia uwepo wa kamati/idara hiyo basi atapaswa kufuata utaratibu kama ulivyo ainishwa kwenye 4(iii),(b),(bb) ya katiba hii.
(9).Fedha yoyote itakayopatikana kwenye mashindano,tamasha,bonanza,ligi au chanzo chochote ikiwemo fedha kutoka utawala wa juu wa chuo au serikali ya wanafunzi  zitakuwa chini ya wizara husika (wizara ya michezo au burudani) kwa kusaidiana na mweka hazina wa kamati au idara husika.
(10). Mwalimu wa michezo au burudani atapaswa kushirikiana na wizara ya michezo/burudani kabla ya kuchukua maamuzi yeyote yale.
(11).Wizara ya michezo/burudani itakuwa na jukumu la kuifadhi na kukarabati vifaa au zana zote za michezo.
17.AFYA NA MAKAZI.
(1).Hairuhusiwi kwa wanafunzi zaidi ya wanne kuishi chumba kimoja.
(2).Wanafunzi wenye jinsia tofauti hawaruhusiwi kuishi wala kulala chumba kimoja.
(3).Kiongozi/viongozi wa hosteli watachaguliwa na wanafunzi wakazi wa hosteli husika chini ya usimamizi wa wizara husika.
(4).Viongozi wa hosteli watawajibika kwa wanafunzi na wizara husika.
(5).Kila mwisho wa mwezi kisima/visima vya maji safi na vyombo vya kuifadhia maji  vitapaswa kufanyiwia usafi pamoja na kuwekwa dawa.
(6). Mwanafunzi anayeishi hosteli au mtu mwingine yeyote haruhusiwi kulewa,kutumia  au kuwa na harufu yoyote ya pombe,sigara, bangi, au madawa yoyote ya kulevya katika mazingira au maisha ya hosteli.
(7).Utawala wa juu wa chuo unapaswa kuhakikisha ya kwamba miundombinu yote ya hosteli iko salama na inakidhi mahitaji,miundombinu hiyo ya weza kuwa;
(a)   Milango,geti,madirisha,sakafu,vioo, pia vitanda au
(b)    Huduma ya maji au umeme.
(8).Utawala wa juu wa chuo utapaswa kuhakikisha ya kwamba maeneo ya chuo ni masafi pamoja na miundombinu yake ikiwemo vyoo,ukumbi na madarasa,zoezi la ufanyaji wa Usafi halitapaswa kufanywa na wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji  Arusha.
(a)   Bila kuathiri masharti yeyote ya katiba hii ,kifungu hicho hapo juu hakihusiki kwa mazingira ya hosteli ambako wanafunzi watalazimika kufanya Usafi wenyewe.







SURA YA NNE.
MAADILI YA WANAFUNZI,VIONGOZI, WALIMU NA WAJIBU.
SEHEMU YA KWANZA
18. MAADILI YA WANAFUNZI
(1)Mwanafunzi atapaswa kufanya ya fuatayo;
(a)   kuheshimu, katiba hii na katiba ya utawala wa juu wa chuo,sheria na kanuni zote za chuo.
(b)   Kuwaheshimu wanafunzi wenzake, walimu, na wafanyakazi wote wa chuo.
(c)    Kuvaa mavazi yenye maadili ya chuo, na kitanzania awapo chuoni au popote pale kwa ajili ya maswala ya kitaaluma au akikiwakilisha chuo,
(d)   Kuvaa aina ya mavazi kwa mujibu wa taratibu za chuo kwa siku husika,yaani kama ni siku ya mavazi ya chuo au kama ni mavazi yeyote.
 (2)Mwanafunzi hatapaswa kufanya yafwatayo;
(a)   Kuiba mali au kitu chochote cha mwanafunzi au chuo ama kwa yeyote,
(b)   Kudharau mwanafunzi yeyote au mwalimu ama mfanyakazi wa chuo,
(c)    Kufanya vitendo vya kiburi,
(d)   Kukidhalilisha chuo ndani au nje ya chuo,
(e)   Kutenda mambo maovu akiwa chuoni au amevaa mavazi yanayokitambulisha chuo au akiwa na nembo yoyote ya chuo popote pale,
(f)     Kubugudhi wanafunzi wenzake wakiwa katika hali ya utulivu wakati wakusoma au katika mazingira ya hosteli,
(g)   Kusema au kutetea uongo na uovu,masengenyo kwa yeyote au vitendo vya udhalilishaji au udhalilishaji  wa kijinsia na uchochezi.
(h)   Kuvaa mavazi yasiyoendana na maadili ya taaluma ya habari na yenye kudhalilisha utu na jinsia yake.
(aa) Kwa mwanafunzi yeyote hatoruhusiwa kuvaa mavazi yatakayokuwa yameishia juu ya magoti na
(bb) Mavazi yenye kuonesha maumbile ya mwili yenye kupaswa kusitiriwa,
(cc) Mwanafunzi yeyote hatoruhusiwa kuva vazi chini ya kiuno,


19.MAADILI YA WALIMU KWA WANAFUNZI.
(1)Mwalimu yeyote wa chuo hiki atapaswa kuwaheshimu wanafunzi wa chuo hiki, na kuepuka vitendo vifwatavyo;
(a)   Lugha zisizo na maadili ikiwemo zenye dharau,kejeli na matusi,
(b)   Uzalilishaji, au kumfanya mwanafunzi apoteze heshima yake mbele ya wengine
(c)    Kumpiga mwanafunzi aidha kwa kutumia fimbo (kumchapa),makonzi,ngumi,makofi na kadhaalika,
(d)   Uchochezi.
 (2)Mwalimu yeyote hataruhusiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi,kujamiiana au uchumba na mwanafunzi wa chuo hiki,bila ridhaa maalumu ambayo itahusisha swala la uchumba tu, utaratibu ufuatao ndio utakao tumika;
(a)   Taarifa za uchumba zifikishwe kwa mlezi wa wanafunzi na waziri wa maadili wa serikali ya wanafunzi, pamoja na mkurugenzi wa chuo.
(b)   Mlezi wa wanafunzi kwa kushirikiana na waziri wa maadili watapaswa kufikisha taarifa kwa wazazi au mlezi/walezi /mfadhili au mdhamini wa mwanafunzi.Kama mwanafunzi huyu hana wazazi au mlezi/walezi /mfadhili au mdhamini basi taarifa zapaswa kwenda kwa ndugu zake.
(c)    Baada ya hatua hiyo wanafunzi wote watatangaziwa uhusiano huo.
(3)Mwalimu hataruhusiwa kuvaa mavazi yatakayo kwenda kinyume na maadili ya kitanzani awapo katika eneo la chuo au popote atakapokuwa akitekeleza majukumu yake kwa mwanafunzi.
(4) Mwalimu hatoruhusiwa kutoza fedha za masomo ya ziada au kwaajili ya shuhuli yoyote ile kutoka kwa mwanafunzi au mfadhili wake kinyume na uratibu uliopo kwenye fomu au mkataba wa malipo,aidha yawe ni makubaiano ya hiyari na wanafunzi husika.
(5)Bila kuathiri mashariti yoyote ya katiba hii,katiba ya utawala,sheria na kanuni nyinginezo; mwalimu hataruhusiwa kufundisha au kutoa kazi kinyume na ratiba au taratibu za chuo au kitaaluma bila kukubaliana na wanafunzi,masomo hayo yatakuwa ni yahiyari.
(6)Kwa mwalimu yeyote atakayekiuka mashariti yoyote yaliyopo kwenye katiba hii,sheria au kanuni;malalamiko yanapaswa kupelekwa kwa mlezi wa wanafunzi.Mlezi wa wanafunzi atapaswa kuyachukulia hatua au kupeleka kwa mnadhimu wa chuo (utwala wa juu wa chuo) au kwenye idara au ngazi nyingine husika za utawala wa juu wa chuo.


20.MAADILI KWA VIONGOZI WA WANAFUNZI.
(1) (mahali popote katika katiba hii neno viongozi wa wanafunzi linamana ya kiongozi yeyote ambaye ni mwanafunzi aliyechaguliwa au kuteuliwa kwa ajili ya kuwaongoza wanafunzi popote pale katika chuo hiki)
Madaraka anayopewa kiongozi wa wanafunzi ni dhamana na atatumia madaraka hayo na kutekeleza wajibu wake kwa:
(a)   kuzingatia masharti ya Katiba hii,kanuni na sheria nyinginezo;
(b)   kuheshimu wanafunzi,walimu na wafanyakazi wote wa chuo, viongozi wenzake na ofisi anayoitumikia;
(c)    Pia  kulinda mali zote za chuo na wanafunzi,
(d)   kukuza imani na heshima ya ofisi kwa wanafunzi;
(2) Ni wajibu  kwa kiongozi kuwatumikia wanafunzi  dhamana ya uongozi na heshima kwa kiongozi wa wanafunzi itazingatia mambo yafuatayo: ‐  
(a) uteuzi kwa misingi ya mwenendo wa mtu, uwezo, sifa au uchaguzi uliyo huru na haki;
(b) uwezo pasipo upendeleo katika kufanya uamuzi na kuhakikisha kwamba uamuzi haufuati undugu, ukabila, udini, upendeleo, rushwa au vigezo vingine visivyo sahihi;
(c) utoaji wa huduma pasipo upendeleo na kwa kufuata maslahi ya wanafunzi kwa kuonyesha-
(aa) uaminifu katika utekelezaji wa kazi za wanafunzi/chuo;
(bb) wajibu wa kutangaza maslahi binafsi ili kuepuka
mgongano wa maslahi;
(d) uwajibikaji kwa wanafunzi katika kufanya uamuzi na vitendo; na  nidhamu na kujituma katika kutoa huduma kwa wanafunzi.
(3)Kanuni za Uongozi kwa  kiongozi wa wanafunzi, akiwa ama katika kazi za ofisi au kazi binafsi au wakati amejumuika na watu wengine, atahakikisha kwamba mwenendo wake:
(a) hauruhusu kutokea mgongano wa maslahi kati ya
maslahi binafsi na maslahi ya uongozi wa wanafunzi;
             (b) hauhatarishi maslahi ya wanafunzi kwa ajili ya maslahi
binafsi; au
(c) haushushi hadhi ya ofisi anayofanyia kazi,wanafunzi au chuo.
(4) Baraza la mawaziri litapaswa kutunga kanuni zaidi zitakazosimamia maadili ya viongozi wa wanafunzi.
 (5) Itakuwa ni marufuku kwa Kiongozi yeyote wa wa wanafunzi, kushiriki kuongeza au kwa namna yoyote ile, kuboresha maslahi yanayohusu wadhifa alionao, na endapo atashiriki, basi masharti hayo mapya yataanza kutumika kwa Kiongozi atakayekuja baada ya yeye kuondoka au kumaliza muda wa kukaa madarakani, kama sivyo mfumo ufuatao wapaswa kutumika;
(a)   Kama ni bunge litapaswa kupata kibali kutoka kwa baraza la katiba na sheria,
(b)   Kama ni baraza la katiba na sheria au serikali ya wanafunzi,kibali kitapatikana kutoka kwa bunge.
(6) Kiongozi wa wanafunzi hataruhusiwa kushika nyadhifa mbili au zaidi au kutumikia Mihimili ya uongozi zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja; yaani bunge la wanafunzi,baraza la katiba na sheria au serikali ya wanafunzi.
(7)Matumizi ya mali ya wanafunzi/chuo
(a)   Haitaruhusiwa kwa Kiongozi yeyote wa wanafunzi kutumia au kuruhusu kutumika kwa mali yoyote ya wanafunzi/chuo, zikiwemo zilizokodishwa kwa Serikali,bunge au baraza la katiba na sheria au chuo, kwa madhumuni ya kumpatia yeye binafsi au mtu mwingine yeyote manufaa ya kiuchumi.
 (8)Miiko yauongozi kwa kiongozi wa wanafunzi.
(a)   Bila ya kuathiri masharti yoyote ya Katiba hii, kiongozi yeyote wa wanafunzi atapaswa kuheshimu na kutii maadili ya viongozi wa wanafunzi, ikiwemo Miiko ya Uongozi, itakuwa kama ifuatavyo:
(9 Kiongozi wa wanafunzi hatopaswa:
(a)   kuvunja au kukiuka masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
(b)   kutoa au kupokea rushwa;
(c)    kujilimbikizia mali kinyume cha sheria;
(d)   kusema uongo au kutoa taarifa zisizo za ukweli;
(e)   kutoa siri za Serikali kinyume cha sheria;
(f)     kutumia wadhifa, nafasi au cheo chake kwa manufaa yake binafsi, familia yake, ndugu, jamaa au marafiki zake au mtu yeyote aliye na uhusiano naye wa karibu;
(g)   kufanya vitendo vya uzembe, uvivu, ubaguzi, kiburi, dharau au unyanyasaji wa kijinsia.
 (10) Kiongozi wa wanafunzi atapaswa:
(a)   kuheshimu na kuendeleza dhana ya uwajibikaji wa pamoja, kwa viongozi wanaohusika; na
(b)   kuheshimu na kuendeleza maadili ya viongozi wa
wanafunzi, ikijumuisha:
 (aa) kuwa na tabia na mienendo inayokubalika katika jamii;
 (bb) kuheshimu, kutunza na kulinda mali za Wanafunzi/chuo; na
 (cc) kutambua, kuheshimu na kuzingatia Kanuni za Maadili na Mienendo ya
Viongozi wa wanafunzi, Kanuni za Kudumu za viongozi wa wanafunzi na miongozo mbalimbali ya Serikali na bunge la wanafunzi kuhusu viongozi wa wanafunzi.
 (11) Kiongozi yeyote wa wanafunzi ambaye anatuhumiwa na kuthibitika kwa makosa ya:
(a) kimaadili;
(b) udhalilishaji wa mtu au wa kijinsia; pia
 (c) wizi au ubadhirifu wa mali za wanafunzi/chuo 
 (d)Au ufuska
atasimamishwa uongozi mpaka suala lake litakapoamuliwa kwa mujibu wa sheria au taratibu nyingine zinazowahusu viongozi wa wanafunzi.
(12)Mara baada ya uchunguzi kukamilika ,kama atakutwa na hatia anaweza;
(a)   Kuvuliwa madaraka,
(b)   Kushushwa cheo,
(c)    Au kuomba radhi,
Kila hatua ya adhabu itachukuliwa kulingana na uzito wa kosa.


SEHEMU YA PILI
21.WAJIBU  WA MWANAFUNZI.
(1)Kila mwanafunzi wa chuo hiki anapaswa kuzingatia yafuatayo;
(a)   kuja chuoni kwa wakati na kuondoka kwa wakati ,
(b)   Kuzingatia ratiba zote za chuo,
(c)    Kufanya majaribio na mitihani kwa usahihi na kwa wakati,
(d)   Kushiriki shughuli mbalimbali za kimasomo
(e)   Kutoa ushirikiano chanya katika jambo lolote lenye maendeleo aidha kwa chuo au maendeleo binafsi, kwa walimu, wanafunzi wenzake, viongozi wa wanafunzi au kiongozi yeyote wa chuo pia wageni,
(f)     Kuwa watulivu wawapo darasani au sehemu yeyote ya mafunzo  aidha ya nadharia ua vitendo,
(g)   Kutoa ushirikiano wa kutosha kwa mwalimu/mkufunzi  au mtu mwingine yeyote aliyepewa dhamana hii kwa muda huo punde awapo katika mafunzo,
(h)   Kutii na kuheshimu katiba hii,katiba ya utawala,sheria, kanuni au taratibu zote halali za chuo au serikali ya wanafunzi.
(i)     Kuishi na wanafunzi wenzake,walimu, viongozi wa wanafunzi,au kiongozi na mfanyakazi yeyote wa chuo; Kwa amani, upendo na kwa kuheshimiana.

 (2) Bila kuadhiri mashariti yoyote ya katiba hii,mwanafunzi yeyote atakayekuwa na sababu ya msingi itakayomfanya asitekeleze wajibu wake kwa ufanisi atapaswa kuomba ruhusa au kutoa taarifa kwa mamlaka husika.
22.WAJIBU WA MWALIMU KWA MWANAFUNZI.
(1) Mwalimu yeyote wa chuo hiki hanabudi kutekeleza wajibu ufuatao;
(a)   Kufundisha kwa wakati na kwa utimilifu,
(b)   Kutoa mazoezi na mitihani kwa mujibu wa mtaala,
(c)    Kuhakikisha wanafunzi wanaelewa anachokifundisha,
(d)   Kujenga na kudumisha amani,umoja nidhamu na mshikamano kwa wanafunzi na walimu dhidi ya wanafunzi,
(e)   Kuhakikisha viongozi wa wanafunzi wanatekeleza wajibu wao kikamilifu,
(f)     Kutekeleza wajibu wao kama walezi na washauri wakuu wa wanafunzi,
(g)   Kusimamia shuhuli zote za kila siku za chuo


SURA YA TANO
ULEZI WA DARASA,UCHAGUZI NA UDHIBITI WA MATUMIZA MABAYA YA FEDHA.
SEHEM YA KWANZA
23. MWALIMU WA DARASA
(i)Kutakuwa na mwalimu wa darasa ambaye atakuwa ndyie mlezi mkuu wa darasa.
(ii)Mwalimu huyu atateuliwa na utawala wa juu wa chuo kupitia uataratibu watakaouweka.
(iii)Kama darasa halitaridhishwa na utendaji au uwepo wa mwalimu huyu kutokana na sababu za msingi, watapaswa kupeleka malalamiko yao kwa waziri wa elimu atakayekuwa na jukumu la kuyafikisha kwa mlezi wa wanafunzi ambayeatayajadili na akiona yana mashiko atayafikisha kwenye idara yenye dhamana husika ya utawala wa juu wa chuo.
(iv) Majukumu ya mwalimu wa darasa.
(a)   Kuhakiki maudhurio ya darasa lake,
(b)   Kuhakikisha darasa lake lina nidhamu,
(c)    Kutekeleza wajibu wake kama mlezi na mshauri mkuu wa darasa husika,
(d)   Kusikili za kero za wanadarasa, maoni maombi na mapendekezo na kuyafanyia kazi au kuyafikisha sehemu husika,
(e)   Kuhakikisha darasa husika linafundishwa kwa kiwango na ubora unaostahiki,
(f)     Kujua udhaifu na ubora wakila mwanafunzi ili kujua jinsi ya kuwasidia na kuwafanya watimize malengo yao yakitaaluma,
(g)   Utatuzi wa migogoro au kutokuelewana baina ya wanadarasa wake au na pande nyingine uko chini yake kama mlezi mkuu,
(h)   Anapaswa kujenga au kudumisha amani,upendo mshikamano na na umoja baina ya wanadarasa na wanafunzi wengine pia dhidi yao na walimu.



SEHEMU YA PILI
24.WAWAKILISHI WA DARASA.
(1)Kutakuwa na viongozi wawili  kwa kila darasa , viongozi hawa wanaweza kuwa wajinsia tofauti au moja kutokana na utashi wa darasa.Watawajibika kwa darasa husika,mwalimu wa darasa,wizara ya elimu na kwa kiongozi mkuu wa serikali ya wanafunzi.
(2) Watachaguliwa na darasa kwa Utaratibu wa upigaji kura.
(3) Kwaa darasa jipya litapaswa kufanya uchaguzi huu baada ya muda wa mwezi mmoja mara baada ya kuwasili chuoni,ila kwa kipindi hicho cha kabla ya mwezi moja wanaweza kumteua/kuwateua viongozi wa muda mfupi.)
(4) Majukumu ya Mwakilishi wa darasa.
(a)   Kufanya shughuli zote kama alivyoagizwa na mwalimu,darasa au viongozi wengine  wa wanafunzi kwa niaba au kwa ajili ya wanafunzi wa darasa lake.
(b)   Kuzikusanya kazi za wanadarasa na kuzipeleka kwa mwalimu pia kuzirejesha.
(c)    Kupeleka malalamiko,madukuduku,maombi au maoni ya wanadarasa kwenye mamlaka husika.
(d)   Kujenga au kudumisha umoja na mshikamano kwa wanadarasa.
(e)   Kutatua migogoro au kutokuelewana baina ya wanadarasa,au darasa lake dhidi ya darasa jingine,mwanafunzi au dhidhi ya mwalimu.
(f)     Kuhakiki maudhurio ya wanadarasa na kutoa taarifa kwa mwalimu wa darasa au mamlaka nyingine husika.
(g)   Kuhakikisha ratiba ya msomo inafuatwa ikiwezekana kumfuata mwalimu wa somo husika.
 (5)Kikao chochote atakachohudhuria au taarifa yoyote atakayopewa atapaswa kuitoa au kutoa maudhui yake kwa wanadarasa.
(6)Hatoruhusiwa kuchukua maamuzi yoyote yale yenye maamuzi makubwa kwa wanadarsa bila kuwashirikisha kwanza.
SEHEMU YA TATU
25.TUME HURU YA UCHAGUZI YA  WANAFUNZI WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA.
(1)Kutakuwa na tume huru ya uchaguzi ya wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha amabayo kiongozi wake mkuu atakuwa ni mwenyekiti wa tume hiyo.
(2) Bunge litapaswa kutunga sheria zitakazoonesha mfumo na muundo wa tume,majukumu ya viongozi na idadi ya wajumbe watume.
(3)Baadhi ya majukumu yake.
(a)   Kuandaa chaguzi huru na za haki,
(b)   Kusimamia kampeni za uchaguzi,
(c)    Kuhakiki vigezo na sifa za wagombea au waliomba katika nafasi husika,
(4) Sifa na vigezo vya wagombea wa nafasi ya Ubunge,Katibu wa wanafunzi,Makamu wa Rais,Afisa uhusiano  na Spika wa Bunge.
(a)   Awe ni mwanafunzi wa chuo hiki,
(b)   Asiwe na sifa ya kufanya kosa/makosa mkubwa yaliyomsababisha kutumikia adhabu kuanzia ya miezi miwili.Adhabu hiyo pamoja na kosa husika linapaswa kuthibitishwa na Baraza la sheria na katiba ngazi ya juu ya kwamba ni sahihi kama sivyo kipengele hiki hakitatumika kama pingamizi,
(c)    Asiwe na hatia ya kutoa mimba,wizi,ufuska pamoja na vitendo vya ulevi vilivyokithiri au matumizi ya madawa ya kulevya.
(d)   Asiwe mlarushwa wala mtoarushwa
(e)   Muda wake wa masomo uliosalia uwe ni kuanzia miezi sita kwaanzia tarehe ya uchaguzi kufanyika ,
(5) Sifa na vigezo vya mgombea wa nafasi ya Urais.
(a)   Sifa na vigezo vyote vilivyopo kwenye ibara 25(4) vitatumika kama vigezo na sifa kwenye nafasi hii ya Urais.
(b)   Vigezo na sifa za ziada;
 (aa) Ngazi yake ya kitaaluma ianzie ngazi ya tano (level five),
(bb)Awe na uzoefu wa uongozi wa kuongoza watu zaidi ya mia moja, waweza kuwa ukiranja pindi alipo kuwa sekondari au katika serikali yeyote ya wanafunzi pia yaweza kuwa wadhifa katika taasisi yoyote inayotambulika kisheria.
(6)Utaratibu utakaotumika ili kuwapata viongozi wa nafasi ya Uraisi,Makamu wa Raisi,Katibu na Afisa uhusiano wa wanafunzi katika uongozi wa serikali ya wanafunzi.
(a)   Tume huru ya uchaguzi itapaswa kutangaza nafasi hizo na kutoa fomu kwa wahusika.Zoezi la uchukuaji fomu litakuwa ni la kipindi cha siku kumi.
(b)   Tume itazihakiki fomu hizo ili kujiridhisha kama wahusika wamekidhi vigezo na sifa za nafasi hiyo.
(c)    Wagombea waliopitishwa na tume wataanza kampeni za uchaguzi kwa kipindi cha wiki moja.Tume ya uchaguzi itapaswa kuhakikisha ya kwamba kampeni hizi haziwagawi wanafunzi wala wagombea kutokana na itikadi za,kikabila,kidini,vyama vya siasa wala kumdhalilisha mtu yeyote.Pia mgombea ataruhusiwa kuwa na meneja wake wa kampeni atakayekuwa na uwezo wa kumpigia kampeni na hata kumwakilisha mgombea.
(d)   Uchaguzi utafanyika katika sehemu ambayo haitajenga mashaka wala hofu kwa wagombea au wanafunzi.Katika uchaguzi huu kila mgombea atachagua wakala wake atakayesimamia  zoezi la kupiga kura na kuhesabu kura.
(e)   Tume itamtangaza mgombea aliyepata kura nyingi kuwa mshindi.
(8)Ukomo wa viongozi/wajumbe wa tume ya katiba utafika pale kiongozi atakapo hitimu masomo yake,kujiuzulu au kuondolewa madarakani au tume kuvunjwa na bunge.
SEHEMU YA NNE
26.MKAGUZI WA HESABU NA MATUMIZI YA FEDHA ZA VIONGOZI WA WANAFUNZI.
(1)Kutakuwa na idara ya mkaguzi wa hesabu na matumizi ya fedha za wanafunzi itakayowajibika kwa bunge la wanafunzi na viongozi wake kuteuliwa na bunge.
(2) Itakuwa na viongozi wakuu watatu ambo ni.
(a)   Mkaguzi Mkuu  ,
(b)   Mkaguzi msaidizi na
(c)    Katibu.
(3)Majukumu ya idara hii.
(a)   Kukagua na kuhakiki matumizi na mapato yote ya fedha kwa viongozi wote wa Bunge,Serikali na Baraza la sheria na katiba, katika ngazi zote yaani wizara,idara na kila ngazia  au cheo.
(b)   Ndio watunzaji wa fedha za serikali ya wanafunzi kwa niaba ya wizara ya fedha ,wanaweza kuziifadhi kwa mhasibu mkuu wa chuo au kwa Utaratibu wataouweka.
(c)    Kwa shirikiana na wizara ya fedha, wanawajibu wa kufuailia ulipaji wa fedha za serikali ya wanafunzi kwa kupitia tarifa za malipo kutoka kwenye mamlaka husika
(d)   Wanawajibu wa kutoa fedha kwa utaratibu maalumu ama watakavyopata kibali kutoka kwa waziri wa fedha.
(e)   Mara baada ya ukaguzi watapaswa kuto taarifa yao kwa bunge na wanafunzi.



Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company