AMISOM wameuteka mji Koryoley, Somalia


Al Shabaab
Wanajeshi wa Muungano wa Afrika wanameuteka mji muhimu wa Koryoley, ulio umbali wa kilomita 90 Kusini Magharibi mwa mji mkuu Mogadishu.
Mji wa Koryoley, umekuwa chini ya udhibiti wa kundi la wanamgambo la Al Shabaab kwa miaka mitano iliyopita.
Mwandishi wa BBC aliye katika eneo hilo anasema kulikuwa mlio wa silaha na baadhi ya raia wa mji wamekimbia.
Kutekwa kwa mji huo ni ukombozi tangu kuanza harakati hizo dhidi ya Al Shabaab mwezi Machi mwaka jana wakiungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Wanajeshi hao wamefanikiwa kukomboa miji mingine muhimu na hata kuwatimua wapiganaji hao kutoka katika ngome zao kubwa.

Wengi wa wanajeshi wa AU ni kutoka Uganda, wakisaidiwa na wanajeshi wa Kenya, Burundi na sasa Ethiopia pamoja na wanajeshi wa Somalia.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company