
Kuongezeka kwa posho hiyo ingawa kihesabu imebaki vilevile sh 300,000 kwa siku kunatokana na Ikulu kubariki pendekezo la uongozi wa Bunge Maalum la Katiba kutaka posho ya kujikimu ambayo ilikuwa sh 80,000 iwe posho ya kikao na ile ya kazi maalumu ya sh 220,000 iwe posho ya kujikimu.
Kabla ya mageuzi hayo, siku za Jumamosi na Jumapili wajumbe walikuwa wakilipwa sh 80,000 kama posho ya kujikimu, lakini kuanzia sasa watalipwa sh 220,000 ambayo imegeuzwa kuwa posho ya kujikimu na ile 80,000 iliyokuwa ya kujikimu imegeuzwa kuwa ya kikao.