Pistorius aanza kujitetea mahakamani,machjozi ya tawala,Mama mkwe haja GUSWA,Dada yake nae alia


Oscar Pistorius akilia alipokuwa chumba cha mahakama Februari 2013
Oscar Pistorius akiwa amejaa majonzi ameanza kutoa utetezi wake katika kesi ya mauaji inayomkabili kwa kuwaomba radhi familia ya rafiki yake wa kike aliyeuawa Reeva Steenkamp.

Kwa sauti ya kutetema, amesema alikuwa "akijaribu kumlinda" na amesema anashindwa kujua uchungu wanaoupata.
Bwana Pistorius amesema anasumbuliwa na"ndoto za kutisha" na mara nyingi aliamka na kusikia harufu ya damu ya Bi Steenkamp.

Waendesha mashitaka wanasema Pistorius alimuua Steenkamp mwezi Februari 2013 baada ya kuzozana. Pistorius anasema alidhani ni jambazi.

Mwanaridha huyo mwenye ulemavu wa miguu amewaambia ndugu wa Bi Steenkamp kwamba "hakuna wakati ambao ameshindwa kufikiria juu yao tangu mkasa huu utokee".

"Naamka kila siku asubuhi na ninyi ni watu wa kwanza kuwafikiria, watu wa kwanza ninaowaombea. Sifahamu uchungu na mawazo na ukiwa ambao nimewasababishia ninyi na familia yenu.

" Nilikuwa najaribu kumlinda Reeva. Nawahakikishia kuwa alipokwenda kulala usiku ule alihisi kupendwa".

"nimejaribu kuandika maneno yangu mengi kwenye karatasi. Mara nyingi kuwaandikia. Lakini hakuna maneno yatakayotosheleza maelezo yangu."

Amesema anatumia dawa za kuzuia msongo wa akili na kukosa usingizi.

"Naogopa kulala, Nimekuwa na ndoto za kutisha, Nasikia harufu ya damu na kuamka nikiwa mwoga.," amesema.

Amesema kamwe hataki kumiliki silaha.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company