MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2014 AKABIDHIWA ZAWADI YAKE WILAYANI UKEREWE MWANZA

Mama Shujaa wa Chakula 2014 Bahati Muriga akitoa neno la Shukurani Baada ya Kukabidhiwa zawadi rasmi zawadi zake Wilayani kwake Ukerewe

Eluka Kibona kutoka Oxfam akimkabidhi ufunguo wa Pikipiki Mshindi wa Mama shujaa wa Chakula


Mama
Shujaa wa Chakula 2014 Bahati Muriga akisaini kupokea zawadi zake
kutoka OXFAM kupitia Programu ya GROW, Wekeza kwa wakulima wadogo wadogo
Inalipa.

Bwana
Hamis Kombo muwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe akitoa salamu za
pongezi kwa Mama Shujaa wa Chakula 2014 pia kuwashukuru OXFAM kwa kutoa
zawadi hizo.

Bahati Muriga akijaribisha kuiwasha Pikipiki yake Mara baada ya Kukabidhiwa

Bahati Muriga akifurahia zawadi zake



Kulwa Kizenga wa kwanza kushoto na Eluka Kibona kutoka OXFAM wakimkabidhi zawadi Bahati Muriga

Mkamiti Mgawe wa kwanza kushoto kutoka OXFAM akiwa na Mama shujaa wa Chakulaa

Zawadi alizopokea Mama Shujaa wa Chakula.

Mshindi
wa Maisha Plus/Mama shujaa wa chakula msimu wa tatu 2014 Bahati Jacob Muriga jana
alikabidhiwa zawadi nyumbani kwake
Ukerewe. Zawadi hizo ni vifaa vya kilimo vyenye thamani ya shilingi
milioni 20 ambapo Bahati Muriga alichagua kununua shamba lenye ukubwa wa ekari
7, pikipiki yenye miguu mitatu aina ya TOYO, vifaa vya kulimo kama vile mbegu,
mbolea, mipira ya kumwagilia, watering cane, water pump, spray pump, koleo na
dawa za kuondoa wadudu na ukungu, majembe, mundu, engine oil lita 2 na petroli lita 96.


Shindano

la Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula 2014 lilifikia tamati mnamo tar. 18 May, 2014 ambapo Bahati Jacob Muriga ndiye aliyeibuka kidedea wa shindano hilo. Mama shujaa huyu ni mkulima
kutoka Nansio, Ukerewe mkoa wa Mwanza na pia ni mwalimu mkuu shule ya Msingi
Mhozya. Ni mjane mwenye watoto watatu na hutumia kilimo kama nguzo ya
kuhakikisha mahitaji ya kifamilia yanatimizwa.




Hafla

fupi ya kumkabidhi zawadi zake Bahati zilifanyika katika Ukumbi wa Afro Beach ambapo
watu na wawakilishi mbali mbali kutoka serikalini na mashirika yasiyo ya
kiserikali kama vile Kivulini, EMEDO walihudhuria ili kushuhudia jinsi anavyokabidhiwa zawadi.

Bw.

Kombo, akimuwakilisha mkuu wa wilaya ya Ukerewe alionesha furaha yake kwa mama
shujaa kutoka Ukerewe alisema” Ninayo
furaha kubwa na kama kiongozi kijana kuona wilaya yetu imetoa mshindi wa
shindano kubwa kama hili na kuiweka ukerewe katika historia na ramani ya nchi kuwa, kumbe nasi tunaweza,
najisikia furaha pia kwa ushindi huu kwani toka anaanza huu mchakato wa
kuchukua fomu na kuelekea kijiji cha maisha plus nilikua miongoni mwa niliotoa
ushirikiano mkubwa kwa kutoa ruhusa na araka
zangu za yeye kushiriki katika shindano hili kwani ni mwalimu huyu”
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company