Bendera ya Jumuia ya Afrika Mashariki
Marais wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanakutana leo mjini Nairobi, Kenya baada ya kutofanyika mkutano wa awali uliokuwa umepangwa kufanyika mwezi wa Desemba mwaka jana mjini Nairobi.
Marais wote watano wa nchi wanachama wanatarajiwa kuhudhuria.
Katika mkutano huo Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania anatarajiwa kukabidhiwa Uenyekiti wa Jumuia hiyo kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, wadhifa ambao alikuwa akabidhiwe mwezi Desemba mwaka jana, lakini hakuweza kuhudhuria mkutano huo kutokana na kwenda kutibiwa nchini Marekani.Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania
Marais wote watano wa nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki, Yoweri Museveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda, Pierre Nkurunzinza wa Burundi, Jakaya Kikwete wa Tanzania na mwenyeji wa mkutano Uhuru Kenyatta wa Kenya.
Mbali na masuala ya uhusiano wa kiuchumi, kisiasa na kijamii miongoni mwa mataifa hayo, kujadiliwa katika kikaohicho, pia maombi ya nchi za Sudan Kusini na Somalia kuomba uanachama wa jumuia ya Afrika Mashariki yatajadiliwa.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago