Burkina Faso: mwili wa Thomas Sankara wafukuliwa

Kaburi inayokisiwa kuwa ya Thomas Sankara, rais wa mapinduzi Burkina Faso, ambaye aliuawa mwaka 1987.
RFI/Sébastien Nemeth
Na RFI

Zoezi la kufukua mwili unaokisiwa kuwa wa aliyekua rais wa Burkina Faso Thomas Sankara limeanza Jumatatu wiki hii katika kujaribu kutaka kubainisha ikiwa ni wake. Thomasa Sankara na washirika wake 12 wa karibu waliuawa mwaka 1987.

Zoezi hilo ni ahadi ya serikali mpya ya Burkina Faso, baada ya kuuangushwa kwa utawala wa Blaise Compaore mwishoni mwa mwaka uliyopita.

Mwili unaokisiwa kuwa wa rais wa zamani Thoma Sankara unatazamiwa kufukuliwa leo Jumanne. Miili ya watu wawili ilifukuliwa Jumatatu wiki hii katika makaburi ya Dagnoën katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.

Miili hiyo inatazamiwa kufanyiwa vipimo, ili kuthibitisha iwapo ni ktapatikana mwili wa aliye kuwa rais wa Burkina Faso Thomasa Sankara.

Zoezi hili limesimamiwa na madaktari wawili kutoka Burkina Faso na mmoja kutoka Ufaransa. Madaktari hawa wanashirikiana na polisi ya masuala ya kisayansi kutoka Burkina Faso pamoja na polisi ya taifa.

Mawakili tu na wanafamialia ndio wanaruhusiwa kuhudhuria zoezi hilo. Lakini familia ya rais Thomas Sankara imewakilishwa na wakili. Kwa mujibu wa Blandine Sankara, mmoja wa dada wa Thomas Sankara aliiambia RFI mwishoni mwa wiki iliyopita, kuwa familia yake haitaka kuhudhuria zoezi hilo la ufukuaji wa muili wa thomas Sankara na washirika wake wa karibu.

Waandishi wa habari na mamia ya wadadisi walifika mapema leo Jumatatu katika makaburi ya Dagnoën. Lakini walitakiwa kuwa mbali kidogo na eneo walikozikwa viongozi hao. Kwa mujibu wa mashahidi,zoezi la kufukua miili hiyo limeanzia kwenye makaburi 2 yaliyo pembezoni mwa kaburi la linalokisiwa kuwa la Thomas Sankara. Kaburi linalokisiwa kuwa la kiongozi huyo halijaguswa.

Madaktari watatu wanaoendesha zoezi hilo watachukua chembechembe za mwili huo na kuzipima wakitumia mashine na mbinu za kisasa za DNA ilikubaini kikamilifu iwapo inahusiana na mwili wa Sankara.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company