Maeneo ya utalii nchini Kenya ambapo idadi ya watalii imeshuka kutokana na mashambulizi ya kigaidi
Idadi ya watalii wanaoelekea nchini Kenya ilishuka kwa asilimia 25 katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka 2015, kwa mujibu wa takwimu za bodi ya watalii zikionyesha namna ambavyo sekta hiyo ilivyodidimia kutokana na kusambaa kwa mashambulizi ya wanamgambo wa al-Shabab ambayo yameuwa mamia ya watu.
Utalii ni sekta muhimu ya mapato ya fedha za kigeni kwa taifa hilo la Afrika mashariki kwa wageni kutembelea mbuga za wanyama na fukwe za baharini, lakini miaka miwili ya mashambulizi yamesababisha hoteli za kifahari kufungwa, kupunguza idadi ya ajira na kupelekea sarafu ya nchi hiyo kushuka kwa miaka mitatu na nusu.
Idadi ya watalii imeshuka hadi 284,313 kutoka 381,278 mwezi Januari hadi mwezi Mei mwaka 2014 ambapo idadi imepungua kwa asilimia 25.4 kwa mujibu wa bodi ya utalii Kenya iliyokaririwa na shirika la habari la Reuters. Idadi hiyo inafuatia kushuka kwa asilimia 4.3 mwaka mmoja kabla ya hapo.
Utalii washuka Kenya
Watalii kutoka Uingereza ambao ndio wateja wakubwa idadi ilishuka kwa asilimia 35 na kufikia 36,022 kwa msimu. Watalii wanaowasili kutoka Marekani idadi ilishuka kwa asilimia 22 na kufikia 30,083.
Kenya imekumbwa na mifululizo ya mashambulizi yanayofanywa na wanamgambo wa al-Shabaab wenye makao yao nchini Somalia katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Watu wenye silaha walishambulia jengo lenye maduka mengi ya kifahari-Westgate Mall - mjini Nairobi mwaka 2013, miji ya pwani mwaka 2014 na chuo kikuu cha Garissa mwezi April mwaka huu. Jumla ya zaidi ya watu 400 wameuwawa.
“Harakati hizi za ugaidi zinaendelea kuzorotesha hali ya uwekezaji katika nchi na imechangia kupoteza ajira na kushuka kwa kazi katika idara yetu ya utalii” alisema waziri wa fedha Henry Rotich. Bajeti yake ya mwaka inayoanzia Julai mosi imeweka shilingi bilioni 5.2 sawa na dola milioni 53.4 kwa ajili ya kufufua utalii nchini humo.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago