Mauaji ya walaji ng'ombe India yaibua hasira

Mauaji ya walaji ng'ombe India yaibua hasira

Mkuu wa chama tawala cha India, cha BJP Amit Shah, amewalaumu wanasiasa wanne wa chama hicho kwa kutoa matamshi ya kutatanisha kuhusu ng'ombe na nyama ya mnyama huyo.

Mmoja alitaka hukumu ya kifo, kwa watu wanaochinja ng'ombe; na mwengine alitoa maanani kisa ambapo Muislamu, aliyetuhumiwa kula nyama ya ng'ombe, alichapwa mikwaju na kundi la watu.

Alidunisha tukio hilo akisema kuwa hiyo ilikuwa ni ajali tu.

Katika kipindi cha mwezi juma lilopita, vifo vingine viwili vya Waislamu, vilihusishwa na ghasia za wazalendo wa Kihindu, kuhusu ng'ombe na ulaji wa nyama ya ng'ombe.

Mapema leo dereva mmoja katika jimbo la Kashmir aliaga dunia kufuatia majeraha aliyopata gari lake lilipowashwa motoMauaji ya walaji ng'ombe India yaibua hasira
Wahindu ndio wengi zaidi katika taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu wanaoamini na kuabudu mnyama Ng'ombe.

Kinaya ni kuwa wengi wao pamoja na waislamu na wakristu walio wachache hula nyama ya ng'ombe.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company