Tanesco: Kina cha maji Kidatu hakitatuathiri

Meneja Uhusiano wa shirika hilo, Badra Masoud
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema kupungua cha  kina cha maji katika bwawa la Kidatu hakutaathiri uzalishaji umeme kwa sababu lina vianzio vingi vya kuzalisha nishati hiyo.

Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam jana na Meneja Uhusiano wa shirika hilo, Badra Masoud, alipokuwa akizungumza na NIPASHE ili kujua hatma ya kupungua kwa kina cha maji katika bwawa la Kidatu linalotegemewa kuzalisha umeme.

“Sisi tuna vianzio vingi vya kuzalisha umeme kama gesi, Simbion na vingine, hatutegemei sana mabwawa na hakutaathiri uzalishaji umeme,” alisema Masoud.

Juzi, Kaimu Meneja wa Tanesco katika mitambo ya uzalishaji umeme ya Kidatu, Joseph Lyauu, aliieleza Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ulinzi na Usalama Kilombero mkoani Morogoro kuwa kina cha maji katika bwawa hilo kipo chini.
CHANZO: NIPASHE
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company