leO KATIKA HISTORIA (SOKA)

LE


Mwanzo wa soka unaweza kupatikana katika kila uwanja wa jiografia na historia. Wachina, Wajapani, Wakorea na Waitalia wote walikuwa wakicheza mpira zamani kabla ya enzi zetu. Wagriki na Waromania walitumia michezo hiyo kuwaandaa wapiganaji kabla ya vita. Hata hivyo, ni nchini Uingereza ambapo umbo la soka lilianza kuipuka. Ilianza wakati mashirikisho mawili (Shirikisho la Mpira wa miguu na Mpira waRagbi) yalitawanyika. Shirikisho la kwanza lilibakia Uingereza. Mnamo Oktoba1963,Vilabu 11 vya London vilituma wawakilishi katika mkutano wa Freemason ili kijadili na kuweka kanuni zilizokubalika kusimamia mechi zilizochezwa kati yao. Mkutano huu ulipelekea kuanzisha kwa Shirikisho la Kandanda (Football Association). Miongoni mwa kanuni zilizowekwa ni zile za kukataa utumiaji wa mikono kushika mpira na kunyanganya kwa nguvu. Soka na Ragbi zilitawanyika mnamo tarehe hii. Miaka minane baada ya kuanzishwa, Shirikisho la Kandanda (FA) lilikuwa na wanachama 50. Shindano la kwanza la kandanda lilianza mwaka huo- Kombe la FA- ambalo lilifuatiwa na lile laLigi ya Ubingwa miaka 17 baadaye. Wachezaji wawili wa Kilabu ya Darwin, John Dovena Fergus Suter walikuwa wa kwanza kulipwa kwa mchezo wao. Kitendo hiki kilikuwa mwanzo wa soka ya kulipwa iliyohalalishwa mnamo mwaka wa 1885. Mwamko huu ulipelekea kuanzishwa kwa Mashirikisho ya kitaifa nje ya Uingereza (Great Britain). Baada ya Shirikisho la Kandanda la Uingereza, Mashirikisho yaliyofuatia ni ya Scotland(1873), Whales (1875) na Ireland (1880). Kutokana na ushawishi mkuu wa Uingereza katika mataifa ya Dunia, Soka ilizambaa kote duniani.Mataifa mengi mengine yalianzisha Mashirikisho ya Kandanda kufikia 1904 wakati Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) lilipoanzishwa.Tangia hapo, kandanda ya kimataifa imekuwa ikikua licha ya vikwazo mbalimbali. Kufikia 1912, FIFA ilikuwa na uanachama wa Mashirikisho 21, idadi iliyoongezeka na kufika 36 kufikia 1925. Kufikia 1930- mwaka ambapo kwa mara ya kwanza kulikuwa na mashindano ya Kombe La DuniaFIFA ilikuwa na wanachama 41. Idadi hii ilizidi kuongezeka na kufika 51 mnamo 1938 na 76 kufikia 1950. Baada ya Kongamano la FIFA la mwaka 2000, kulikuwa na wanachama 204 na idadi hii inazidi kukua kila mwaka.
Kanuni
Maagizo ya Kandanda hupitiwa na kufanyiwa mabadiliko kila mwaka (Mwezi wa Julai) na Shirikisho la Kandanda Duniani (FIFA).[1]
Mpangilio wa wachezaji
[2] [3] Kuna wachezaji wa aina tatu: Walinzi, wachezaji wa kiungo na wachezaji wa mbele au straika. Goli kipa au mlinda lango ni mmoja kati ya walinzi. Ni uamuzi wa kochakuhusu idadi ya wachezaji wanaocheza kuwa walinda lango, wa kiungo au wa mbele, ikitegemea mfumo uliotumika. Mfumo wa 4-4-2[4] umekuwa maarufu miongoni mwa timu nyingi. Mfumo huu hujumlisha walinzi wanne pamoja na mlinda lango, wachezaji wanne wa kiungo na wawili wa mbele.
Utunukizi wa Alama
Katika ligi za kitaifa na kimataifa, alama hutunukiwa kwa timu baada ya mchezo. Timu iliyoshinda hupewa alama tatu huku timu zilizotoka sare hupewa alama moja kila moja. Ikiwa ni lazima mshindi apatikane, hasa kwenye meji za finali, mchezo huwa na muda wa ziada kama timu hizo ziko sare. Iwapo sare hiyo huendelea mchezo huamuliwa kwa mikwaju ya penalty.
Shirikisho la Kandanda Duniani
[5] Shirikisho la Soka Duniana (FIFA) ndili shirikisho kuu linalosimamia Kandanda duniani. Wanachama wake ni mashirikisho ya kandanda ya nchi mbalimbali. Kufikia mwaka wa 2000, lilikuwa na wanachama 204 kutoka pembe zote za dunia. Shirikisho hili huandaa mashindano mbalimbali ya soka kama vile Kombe la Dunia na pia huwatunuku wachezaji.
Orodha ya Wachezaji Maarufu Duniani
[6] Orodha ifuatayo inaonyesha baadhi ya wanasoka maarufu Duniani, lakini haiashirii usanjari huu kulingana na ubora. Wapo wengine wengi ambao hawajatajwa hapa.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company