Maelfu ya watu nchini Misri wameandamana mjini Cairo kumuunga mkono rais Mohammed Morsi.


Rais Morsi atakuwa mamlakani kwa miaka mitano

Maandamano hayo yaliandaliwa na chama cha rais Morsi cha Muslim Brotherhood kwa ushirikiano na makundi mengine ya kiisilamu.
Waandamanaji walipiga mayowe wakilaani walichokiita upinzani ambao unapanga maandamano makubwa mwezi huu dhidi ya utawala wa rais Morsi.
Utakuwa ndio mwaka wa kwanza tangu kuingia mamlakani kwa rais Morsi atakayetawala kwa miaka mitano.
Waandamanaji hao wataandamana wakitaka kumshikiza rais Morsi.
Wadadisi wanasema kuwa maandamano ya kumpinga rais Morsi pamoja na yale ya kumuunga mkono ni ishara ya kuonyesha hali ya migawanyiko ilivyo kisiasa nchini Misri zaidi ya miaka miwili baada ya mapinduzi ya kiraia kumuondoa mamlakani aliyekuwa rais Hosni Mubarak.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company