Hali tete na tata ya kituo cha mabasi cha Ubungo (UBT)- Hatua ambazo nimeanza kuzichukua
kwa mujibu ya blogu yake;
www.hakileo.blogspot.comKatika siku za karibuni nimepokea malalamiko kuhusu hali tete na tata
katika Kituo cha Mabasi cha Ubungo (UBT) kinachosimamiwa na kuendeshwa
na Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam.
Kufuatia malalamiko hayo, nimechukua hatua zifuatazo mpaka sasa: Mosi,
tarehe 15 Julai 2013 nilifanya ziara ya ghafla kujionea hali halisi,
sehemu ya ziara hiyo inaweza kutazamwa kupitia:
http://www.youtube.com/watch , ambapo nilibaini kwamba hatua za haraka zinahitajika.
Nimeshuhudia hali ya uchafu ikiwemo utiririkaji wa maji machafu ndani
ya Kituo cha Mabasi ambayo yanatuama na hadi kubadilika rangi na kuwa ya
kijani ambapo ni hatarishi kwa abiria na watu wanaofanya shughuli zao
ndani ya kituo. Pia, kuna vyoo vichache ukilinganisha na idadi ya abiria
na watumiaji wengine wa Kituo. Hali hiyo inaweza kusababisha magonjwa
ya mlipuko.
Nimejulishwa hali ya usalama ndani ya kituo ni tete; usalama ndani ya
kituo ni mdogo sana kwa abiria na nimepewa taarifa za matukio ya uhalifu
ambayo yamesababisha pia madhara kwa abiria.
Nimetembelea kituo na kukuta kuna usumbufu mkubwa sana kwa abiria na
watumiaji wengine wa Kituo baada ya maeneo ya awali ya kupumzikia kwa
abiria na wasindikizaji kubomolewa.