Hatimae 400,000 kurudi kazini leo nchini Marekani

                     
                                                        KWA UFUPI
Hatua hiyo iliyochukuliwa na Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Chuck Hagel iko chini ya sheria ya Marekani inayoitwa Pay Our Military Act ambayo inahimiza malipo kwa wanajeshi.
Washington.Zaidi ya wafanyakazi 400,000 wa Idara ya Ulinzi nchini Marekani waliorejeshwa nyumbani kufuatia kuendelea kufungwa kwa baadhi ya shughuli za Serikali wameombwa kurudi kazini kuanzia leo.



Hatua hiyo iliyochukuliwa na Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Chuck Hagel iko chini ya sheria ya Marekani inayoitwa Pay Our Military Act ambayo inahimiza malipo kwa wanajeshi.


Sheria hiyo ilipitishwa na Bunge na kutiwa saini na Rais Barrack Obama muda mfupi kabla ya kufungwa kwa shughuli hizo za Serikali.


Hatua hiyo ni kufuatia Bunge la nchi hiyo kushindwa kufikia makubaliano kuhusu bajeti.


Obama alisema kuna njia moja tu ambayo inaweza kumaliza hali hii ambayo ni kupitisha bajeti inayogharimia Serikali bila kuegemea upande wowote wa chama.www.hakileo.blogspot.com
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company