Netanyahu asema wapo tayari kusimama peke yao kuzuia utengenezaji wa silaha za nyuklia nchini Iran



Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akihutubia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa UNGA
Na Nurdin Selemani Ramadhani

Serikali ya Israel imetangaza utayari wa kusalia peke yake ili kuendelea kupambana na kitisho cha usalama kutoka kwa Iran wanayoituhumu ipo kwenye harakati za mwisho za kutengeneza bomu la nyuklia na kuyaonya Mataifa ya Magharibi kuacha kumuamini Rais Hassan Rouhani.
Israel imesema itatumia kila mbinu hata kama haitapata ushirikiano kutoka kwa mataifa mengine katika kuhakikisha juhudi za harakati za kutengeneza bomu la nyuklia zinazofanywa na Iran zinamalizwa ili kuhakikisha eneo la Mashariki ya Kati linabaki kuwa salama.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema nchi yake haipo tayari kuruhusu au kuona Iran ikitengeneza silaha za nyuklia na iwapo haitopata ushirikiano katika kuzia hilo wao watasimama peke yao kuhakikisha silaha hizo hazimiliki na Tehran.

Netanyahu ameshangaa ni kwa nini mataifa yamefanya haraka kumuamini Rais Rouhani ambaye alizungumza na Rais wa Marekani Barack Hussein Obama na kueleza utayari wa nchi yake kutoa ushirikiano juu ya mpango wake wa nyuklia.

Kiongozi huyo wa Serikali ya Israel amemtuhumu Rais Rouhani kwa kuifanya dunia kuonekana umepumbazika lakini akasisitiza hawezi akafanikiwa kuipumbaza kwa mara nyingine kwani Jerusalem imeshagundua harakati zote wanazofanya juu ya kutengeneza silaha za nyuklia.

Netanyahu pia amesema njia pekee ya kuendelea kuhakikisha Iran haifanikiwi kwenye mpango wao wa kutengeneza silaha za nyuklia ni kwa kuongeza vikwazo ya kiuchumi dhidi yao na hata kutishia kuishambulia kijeshi.

Waziri Mkuu Netanyahu amesema bila kufanya hivyo hali itakuwa mbaya kwa kuwa Rais Rouhani ametoa matamshi ambayo kwa namna moja ama nyingine hayatotekelezeka kwani msimamo wa nchi hiyo ni kuwa na silaha za kemikali.

Israeli imesema kama itafikia hatua na kulazimika kuishambulia kijeshi Iran bila ya kupata usaidizi itafanya hivyo kwa kuwa hiyo ni sehemu ya kujilinda sanjari na kulinda wananchi wake.

Serikali ya Iran imekosa vikali maneno ya Waziri Mkuu Netanyahu wakisema amekuwa akifanya hila ili kuhakikisha nchi hiyo ionekane haina nia ya kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa katika kusaka sulhu ya mpango wake wa nyuklia.www.hakileo.blogspot.com
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company