Rais wa Marekani Barack Obama ameonya kuhusu madhara ya muda mrefu yanayoweza kutokea kutokana na kufungwa kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka 17 kwa baadhi ya shughuli za serikali. Obama amesema kuwa kundi moja la chama katika bunge la Marekani limesebabisha kufungwa kwa shughuli za serikali ya shirikisho na kwamba kuendelea kwa mkwamo huo kwa muda mrefu , kutaleta matokeo mabaya zaidi .
Ameonya kuwa familia za watu wa kawaida pamoja na shughuli za kibiashara zitaathirika zaidi. Akizungumza kutoka katika Ikulu ya White House katika siku ambayo wafanyakazi laki nane wa serikali wamepewa amri ya kubakia nyumbani, Obama amekilaumu kikundi cha Tea Party katika chama cha Republican kwa kushindwa kwa bunge la Marekani kupitisha sheria ya kurefusha kuigharamia serikali kwa kipindi kifupi kupindukia muda uliokwisha malizika usiku wa manane siku ya Jumatatu.www.hakileo.blogspot.com