Ndugu zangu,
Jana nilifika Neema Craft Cafe hapa Iringa. Mlangoni nikakuta tangazo, kuwa kuna ofa ya kahawa nyeusi ya bure ya kuonja na keki.
Ukweli tangu nianze kutembelea mgahawa wa Neema sijawahi kuagiza kahawa nyeusi.
Ukweli tangu nianze kutembelea mgahawa wa Neema sijawahi kuagiza kahawa nyeusi.
Lakini, kwa vile nimeambiwa siku hiyo kuna ya bure, basi, sikwenda kuagizia chai kama ilivyo kawaida yangu. Nikaenda moja kwa moja kuulizia hiyo kahawa ya bure ya kuonja na keki yake. Nikapewa birika ndogo na keki!
Na meza ya jirani Mtanzania mwenzangu hakujua kuwa kuna ofa hiyo. Alikuwa akila mlo wake wa mchana. Naye nilipomwambia, basi, akanijibu haraka;
" Ok, ok! Ngoja nimalize hapa nami nikaonje hiyo kahawa ya bure na keki!"
" Ok, ok! Ngoja nimalize hapa nami nikaonje hiyo kahawa ya bure na keki!"
Baada ya kikombe kimoja cha kahawa, nikatafakari, kisha nikajisemea, kuwa mimi ni Mtanzania haswa!
Je, nawe unajiona Utanzania wako katika hili, au uko tofauti?!