Shirika la Kimataifa la Waandishi wa Habari na Maripota Wasiokuwa na Mpaka (RSF) limetangaza leo kuwa, jumla ya waandishi wa habari 71 wameuawa katika maeneo mbalimbali duniani mwaka huu wa 2013. Gazeti la Le Figaro linalochapishwa nchini Ufaransa limeandika kuwa, idadi ya waandishi wa habari na maripota waliouawa katika maeneo mbalimbali duniani imepungua mwaka huu ikilinganishwa na mwaka uliopita wa 2012.
Taarifa ya kila mwaka ya RSF imeeleza kuwa, mwaka huu jumla ya waandishi wa habari na maripota 71 wameuawa mwaka huu, ikilinganishwa na waandishi wa habari na maripota 88 waliouawa mwaka jana. Taarifa ya shirika hilo la kimataifa imeongeza kuwa, waandishi wa habari na maripota 87 walitekwa nyara mwaka 2013. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, idadi kubwa ya waandishi wa habari wameuawa katika nchi za Syria, Somalia na Pakistan.