Muda mchache uliopita wabungge wa bunge malumu la katiba wametoka nje ya ukumbi wa bunge mara baada ya mchango wa Profesa Lipumba aliyetamka ya kwamba wamechoshwa na matusi ndani ya bunge hilo.
Mara kwa mara bunge hili limekuwa na mvutano kwa pande mbili amabzo moja hutaka serikali mbili huku upande mwingine ukitaka serikali tatu.
Na jana nilitamka bayana kupitia kwenye blogu hii ya kwamba nimepoteza imani na bunge hilo kutokana na mwenendo wake.
Japo wajumbe hilo wametoka ambao ni wale wa UKAWA yaani Umoja wa Katiba ya Wananchi bado bunge hilo linaendelea.
Kumbuka umoja huu unaundwa na vyama vya upinzani Tanzania na wajumbe wachache wa bunge hli ambao hutoka katika makundi maalumu.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago