MESSI AREJESHA FURAHA BARCELONA, YASHINDA 2-1 LA LIGA



Lionel Messi akishangilia baada ya bao lake la ushindi aliloifungia Barcelona usiku wa jana

NYOTA Lionel Messi amehitimisha dakika 348 za kucheza bila kufunga bao, akiiwezesha Barcelona kushinda mabao 2-1 dhidi ya Athletic Bilbao katika La Liga.

Muargentina huyo alifunga kwa mpira wa adhabu dakika mbili baada ya Pedro had kusawazisha dhidi ya Athletic Bilbao Uwanja wa Nou Camp.

Messi aliyecheza mechi tatu bila kufunga, usiku wa jana alifunga bao lake dakika ya 74 wakati Pedro alifunga dakika ya 72 baada ya wageni kutangulia kupata bao dakika ya 50 kupitia kwa Aduriz.

Barcelona imefikisha pointi 81 baada ya kucheza mechi 34 na inarudi nafasi ya pili, nyuma ya Atletico Madrid yenye pointi 85 za mechi 34 pia, wakati Real Madrid ina pointi 79 za mechi 33 na Jumamosi itacheza na Osasuna
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company