TAIFA STARS yatia doa sherehe za muungano YACHAPWA 3-0 NA BURUNDI

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa stars imechapwa mabao 3-0 dhidi ya Burundi katika mechi ya kirafiki ya kuadhimisha miaka 50 ya muungano, uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam.

Mmechi hiyo imechezeshwa na refa Anthony Ogwayo kutoka Kenya akisaidiwa na Gilbert Cheruiyot na Oliver Odhiambo wote pia kutoka Kenya.

Mwamuzi wa mezani alikuwa Israel Mujuni wa Tanzania wakati Kamishna ni Charles Ndagala.

Mabao ya Burundi yamefungwa na Didier Kavumbagu, Amis Twambwe wanaocheza soka la kulipwa nchini Tanzania.

Bao la tatu la Burundi limefungwa na Yufuf Ndikumana na kuifanya Stars iwahuzunishe watanzania waliokuwa na furaha ya kuadhimisha miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company