WANAUME CHANZO SARATANI YA MLANGO WA UZAZI

Na Hudugu Ng'amilo.
WANAUME wametajwa kuwa chanzo kikuu cha wanawake kupata ugonjwa wa saratani ya mlango wa uzazi ambayo imekuwa tishio kwa sasa.

Mshauri wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la PSI-Tanzania, Dk. Mashafi Joseph, alieleza hayo jijini Dar es Salaam juzi alipozungumza na waandishi wa habari akizungumzia udhamini wao katika Jukwaa la Wanawake la 'Familia Kitchen Party Gala', litakalofanyika Aprili 27, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee kupitia chapa yao ya familia.

Akifafanua hilo, Dk. Mashafi alisema kisayansi wanaume ndio wabebaji wa kirusi kinachosababisha ugonjwa huo kinachoitwa Human Papillomavirus (HPV) ambako kwao hakina madhara ila kinapofika kwa mwanamke ndipo anapata saratani hiyo ambayo huambukizwa kwa njia ya kujamiana.

Kwa hapa nchini alisema saratani hiyo si tu inaongoza kwa vifo vya kina mama bali pia ni aina ya saratani ambayo inakuwa kwa kasi katika nchi za Afrika Mashariki huku Tanzania ikiwa na mzigo mkubwa wa wagonjwa.

Kuhusu udhamini wao kwa jukwaa la 'Familia Kitchen Party Gala', inayoandaliwa na Women Footprints Initiative, alisema wameamua kushirikiana nao kwa lengo la kupunguza vifo vya kina mama vitokanavyo na uzazi.
CHANZO TANZANIA DAIMA
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company