Jeshi la Nigeria
Jeshi nchini Nigeria linasema kuwa linafanya oparesheni ya mwisho kwenye msitu moja ambao unaaminiwa kuwa ngome kuu ya wanamgambo wa Boko Haram.
Msemaji wa jeshi (Chris Olukolade) alithibitisha kuwa opaesheni zinaendelea kwenye msitu wa Sambisa karibu na mpaka na Cameroon.
Serikali ya Nigeria inasema kuwa Boko Haram wako mbioni na jeshi limeapa kuwashinda kabla ya kuapishwa kwa rais mpya Muhammadu Buhari tarehe 29 mwezi Mei.
Inaaminika kuwa zaidi ya wasichana 200 wa shule ambao walitekwa nyara mwaka mmoja uliopita kutoka mji wa Chibok huenda wameshikiliwa ndani ya msitu huo
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago