Ghasia zazuka nchini Burundi
Watu wawili wameripotiwa kuuawa baada ya kupigwa risasi na maafisa wa polisi kufuatia ghasia kati ya polisi na waandamanaji katika mji mkuu wa Bujumbura nchini Burundi.
Waandamanaji wameishtumu serikali kwa kufanya mapinduzi ya kikatiba baada ya uteuzi wa rais Pierre Nkurunziza kupigania muhula wa tatu.Maandamano Burundi
Mwandishi wa BBC anasema kuwa watu wengi wamejeruhiwa huku wengine wakikamatwa.
Maafisa wa polisi walikivamia kituo kimoja cha redio kinachounga mkono upinzani na kutishia kukifunga iwapo hakitasitisha matangazo yake ya moja kwa moja kuhusu maandamano hayo.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago