
Nchimbi aliyelitumikia jimbo hilo kwa miaka 10 alikutana na wanachama wa chama cha mapinduzi Katika uwanja wa majimaji mjini Songeapamoja na kuelezea mafanikio mbalimbali ya maendeleo aliyoyafanya katika jimbo hilo ikiwemo ujenzi wa barabara, zahanati na shule za sekondari lakini pia akatumia nafasi hiyo kutangaza rasmi kutogombea tena ubunge katika jimbo la songea mjini.
Tamko hilo la dkt. Nchimbi lilizua simanzi kwa baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM Songea huku wengine wakishindwa kujizuia na kujikuta wakimwaga machozi.
Katika maelezo yao wanachama hawa walisema kuachia ngazi kwa Dkt, Nchimbi kutogombea katika jimbo hilo kunatoa fursa kubwa kwa vyama vya upinzani kuchukua jimbo hilo hali ambayo hawakubaliani nayo.
Hata hivyo wanachama hao walimuomba mbunge huyo kutengua msimamo wake na kumtaka arejee tena kugombea jimbo la Songea mjini, jibu la dkt. Nchimbi likawa anaenda kufikiria.