Baada ya kuzushiwa kifo ,muimbaji mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Banza Stone amesema si jambo la busara la kuzushiana kifo
Akizungumza kwenye AMPLIFAYA ya Clouds Fm jana june 24 alisema: "Mimi nilikuwa nasumbuliwa na kichwa sana na ki homa homa fulani kama miezi miwili lakini saaa hivi niko vizuri, naelendele poa na leo nilienda hospitali daktari kufanya sound check akaniambia kuwa malaria"
Mtangazaji:…Jana ilikua ni mara ngapi kuzushiwa kifo ?
Banza Stone:.."Mimi hata sijui ila nasikia mara watu oooh banza kafa, mara ooh kila mtu anaongea lake ila mimi niko poa ni mzima naweza kufanya kazi ila kwasasa siko tayari kufanya kazi kwani nitauchosha mwili mwangu"
Mtangazaji: Vipi kuhusu kazi zako za muziki bado unaendelea nazo ama au ??
Banza Stone:….."Naweza kusema ninaendelea na muziki kama kawaida kwasababu sasa hivi nina kama nyimbo sita mpya ziko ndani kesho, kesho kutwa naweza nikaamua niachie moja mpaka video ziko tayari sio za bendi bali ni zangu binafsi…"
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago