SAMS : Syria yaendesha mashambulizi ya kemikali

Kwa mujibu wa ripoti ya SAMS, mabomu ya kemikali yalirushwa kwa helikopta katika vijiji viliyo pembezoni mwa mji wa Idleb.
REUTERS/ Shaam News Network
Na RFI

Kundi la madaktari na waganga wa Syria na Marekani SAMS (Syria American Medical Society), watawasilisha leo Jumatano mbele ya Baraza la wawakilishi la Marekani ushahidi wa matumizi ya silaha za kemikali yanayotekelezwa na serikali ya Syria katika jimbo la Idleb.
     Kwa mujibu wa ripoti hii inayoeleza kinaga ubaga(takwimu, picha, video), utawala wa Assad unasadikiwa kuendesha mashambulizi 31 kwa kutumia kemikali ya klorini kati ya Machi 16 na Juni 9 mwaka 2015.

Ripoti hii inaeleza kuwa mabomu yalirushwa kwa helikopta dhidi ya raia, na kusababisha vifo vya watu kumi. Kwa uchache watu 530 walifanyiwa matibabu, kwa mujibu wa Dk Mohamed Tennari, mratibu wa SAMS,alihojiwa na RFI jijini Washington.

Mwezi Januari mwaka huu, Shirika linalopiga marufuku silaha za kemikali lilielezea wasiwasi wake kuhusu matumizi ya klorini kama silaha ya vita nchini Syria. Kwa mujibu wa ripoti ya Syria American Medical Society (SAMS), mashambulizi hayo bado yanaendelea kushuhudiwa nchini Syria:

" Tumepokea watu wengi walioathirika na silaha za kemikali, watu hawa walikua wakiishi katika vijiji viliyo pembezoni mwa mji wa Idleb na vijiji hivi vilishambuliwa kwa mabomu ya kemikali, ameeleza Dk Mohamed Tennari, mratibu wa SAMS. Mashambulizi haya yalianza mwezi Machi na yaliendelea hadi leo " amesema Dk Mohamed Tennari.

" Mashambulizi 31 ya kemikali yaliendeshwa katika mkoa wa Idleb. Watu walioathirika na mashambulizi hayo wana dalili zinazojulikana, ambazo zinaonekana kwa mtu baada ya kunywa au kumwagiwa kemikali. Dalili hizo ni matatizo ya kupumua, madonda kwenye jicho na kwenye ngozi. Baadhi ya waathirika ni kutoka vijiji viliyo mbali na maeneo yaliyoshambuliwa, hali hii inaonyesha jinsi gani silaha za kemikali zinavyosambaa hadi kufikia maeneo yaliyo mbali zaidi ”, ameongeza Dk Mohamed Tennari.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company