Serikali ya Afghanistan inasema kuwa imefanikiwa kusitisha shambulio katika bunge na kuweza kuwaua washambuliaji wote.
Kundi la wapiganaji wa Taleban limekiri kutekeleza shambulio hilo ambalo lilianza na kulipuka kwa gari lililotegwa vilipuzi nje ya bunge kabla ya ufyatuzi wa roketi na risasi.Bunge
Hatahivyo wapiganaji hao walishindwa kuingia ndani ya jengo la bunge.
Msemaji wa wizara ya ndani amesema kuwa hakuna mbunge aliyejeruhiwa lakini zaidi ya watu 20 walijeruhiwa na vigae vya chupa.
Afisa mmoja wa wizara ya afya amesema kuwa mmoja ya waliojeruhiwa alikuwa katika hali mbaya.Shambulizi Afghanistan
Shambulizi hilo lilifanyika wakati bunge lilipokutana ili kumchagua waziri mpya wa ulinzi.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago