Wapiga kura wamejitokeza kwa wingi. Askari polisi 10,000 wametumwa katika vituo mbalimbali, wakisaidiwa naaskari polisi na wanajeshi 5,000 wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa (MINUSTAH).
REUTERS/Andres Martinez Casares
Na RFI
Wananchi wa Haiti wamepiga kura kwa duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais na pia katika duru ya pili wa uchaguzi wa wabunge, na kwa duru moja tu kwa uchaguzi wa manispaa.
Kumeshuhudia chaguzi nyingi na wagombea wengi. Kwa uchauguzi wa rais pekee, wagombea ni 54 ambao wanawania nafasi ya Michel Martelly. ilikua inatazamiwa kuwa vituo vya kupigia kura vingelifunga saa 2:00 usiku saa za kimataifa. Ushiriki umeongezeka kwa kasi ikilinganishwa na uchaguzi wa mwezi Agosti mwaka jana.
Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, Port-au-Prince, Amélie Baron, katika soko la Canape vert, ambalo linapatikana katikati ya mji mkuu wa Haiti, wapiga kura wameonekana kwa wingi na shughuli zimeendesha kwa utulivu. Hiki ni kituo kikubwa cha kupiga kura na nje na ndani ya kituo hiki, askari polisi wameonekana kwa wingi na maafisa wamekuwa wakiangalia kwamba watu wamebebelea kadi zao za uraia. Ni hatua ambayo imechukua muda, lakini wananchi wamesubiri kwa utulivu na licha ya joto kali, kumeonekana foleni ndefu chini ya jua kali.
Ni tukio ambalo Haiti haijawahi kushuhudia kwa zaidi ya muongo mmoja na hali hiyo imewaridhisha wapiga kura waliojielekeza kupiga kura, lakini pia waandaaji. Celso Amorim, afisa wa Ujumbe wa waangalizi wa OEA, Shirikisho la nchi za Marekaniameridhika na na jinsi wananchi walivyopongeza hali hiyo: " Nimezungumza na baadhi ya wapiga kura ambao wamenambia, tumepiga kura, tuna furaha ya kupiga kura. Hiyo ni muhimu zaidi".
" Kuwa na imani hiyo, ni kuonyesha jinsi gani raia walieleweshwa namna ya kupiga kura kwa utulivu ", ameongeza Amorin. " Vikosi vya usalama, polisi, wamechukua hatua muhimu. Hii inathibitisha kile nimeona na kusikia hadi sasa. Natumaini kuwa hali itaendelea kuwa ya utulivu kama mara ya kwanza ", amemalizia Celso Amorim.
Wakati wa mchana, polisi imekua imesema kuwa imewashikila watu 73 nchini kote. Watu ambao walikutwa wakiwa na kadi nyingi za kupigia kura kwa ruhusa za uongo. Ruhusa Hizi ni nyaraka ambazo vyama vya siasa vimewakabidhi wafuasi wao ili waweze kufuatilia mwenendo sahihi wa zoezi la uchaguzi.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago