kumekucha,BALAA JINGINE

HABARI ZETU

  •  MWALIMU ALIYEMBAKA MWANAFUNZI 'MTEGONI'
  • MAHAKAMA YAMPELEKA GEREZANI MIAKA 30


 Na Nickson Mahundi, Ludewa kwa hisani ya MAJIRAwww.hakileo.blogspot.com

MAHAKAMA ya Wilaya ya Ludewa, mkoani Njombe, imemhukumu kifungo cha miaka 30 gerezani na kuchapwa viboko 30 mwalimu wa Shuile ya Msingi Ingwachanya.


Mwalimu huyo, Bw. Romanus Msango, mkazi wa Lupembe, wilayani Njombe, alitiwa hatiani kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa miaka 14 (jina linahifadhiwa) na kumuumiza vibaya sehemu za siri.

Akisoma hukumu hiyo Septemba 6 mwaka huu, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ludewa, Bw.

Fredrick Lukuna, alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka ambao haukuwa na shaka yoyote.

Alisema mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 1309(1) na 31(1) cha kanuni ya adhabu ya mwaka 2002 hivyo adhabu hiyo ni fundisho kwa wengine.

"Natoa adhabu hii ili kukomesha vitendo hivi kwenye jamii

kwani vinaleta madhara makubwa kwa watoto na wanawake pamoja na kusababisha magonjwa ya kuambukiza," alisema.

Awali ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka, Edison Kasekwa kuwa, mshtakiwa alitenda ukatili huo wa kinyama Agosti 20,2012 katika Kijiji cha Masimbwe, Kata ya Mlangali.

Alisema kabla mshtakiwa hajatenda kosa hilo, alimshambulia mwanafunzi huyo, kumbaka na kumlawiti jambo ambalo lilimsababishia maumivu makali.

"Serikali ilimpa mshtakiwa dhamana kubwa ya kulea watoto ambao ni nguvukazi ya Taifa la kesho lakini amewageuka na kutenda kitendo ambacho ni kinyume na maadili ya kazi yake, kuidharirisha taaluma hivyo naomba mahakama itoe adhabu kali iwe fundisho kwa walimu wengine," alisema.

Bw. Kasekwa aliongeza kuwa, mshtakiwa alikusudia kutenda makosa hayo kwa sababu alimfuata mwanafunzi huyo shambani wakati akivuna mahindi na wenzake ambao walikimbia kwenda kijijini kutoa taarifa baada ya mshtakiwa kumkamata mwenzao na kumpeleka kichakani.

Wa k a t i h u o h u o , wa t u wawili Bahati Mtega na Flowin Mtweve, wote wakazi wa Milo, wamehukumiwa kifungo cha maisha gerezani na kuchapwa viboko 12 kila mmoja kwa kosa la kumbaka mke wa mtu na kumsababishia maumivu makali
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company