Mtu mmoja amekufa na wanne kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu lililotegwa ndani ya basi la abiria katika eneo la Nasr mji mkuu wa nchi hiyo Cairo kufuatia vurugu na mivutano inayoendelea nchini humo kufuatia kundi la Muslim Brotherhood kupigwa marufuku
Taarifa toka katika mji wa Nasr zinaeleza kuwa uchunguzi Zaidi unafanyika ili kujua chanzo cha shambulio hilo la bomu ndani ya basi hilo
Hata hivyo haijajulikana mara moja kama bomu hilo lilikuwa limetengwa ndani ya basi hilo la abiria ama lilirushwa
Mlipuko huu wa bomu unakuja ikiwa ni siku moja baada ya serikali ya Misri kulitangaza kundi la Muslim Brotherhood kuwa ni la kigaidi
Kundi hili la Muslim Brotherhood mgombea wake katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo 2012 Mohammed Morsi alishinda kuwa Rais kabla ya kuondolewa na jeshi la nchi hiyo mapema mwaka huu
Kiongozi wa kundi hilo ambaye kwa sasa yupo kizuizin ameendelea kutoa wito kwa waandamanaji kuendeleza mapambano
Katika miezi ya hivi karibuni Misri imekuwa ikikabiliwa na mfululizo wa mashambulizi yanayodaiwa na serikali ya nchi hiyo kwamba yanatekelezwa na makundi ya wapiganaji wa kiislam
Hata hivyo Serikali ya Misri imeendelea kulaumu Muslim Brotherhood kwa shambulio la bomu lilofanywa Jumaane dhidi ya makao makuu ya polisi katika mji wa Mansoura, kaskazini mwa Cairo na kusababisha vifo vya watu 13.