Kikosi cha kwanza cha kulinda amani Sudan kusini chawasili


kikosi cha umoja wa Mataifa UN kimewasili kulinda amani Sudan Kusini
RFI
Na RFI

Kikosi cha kwanza cha umoja wa mataifa UN cha kulinda amani huko sudan kusini kimewasili jana ijumaa nchini humo wakati huu umoja wa mataifa ukionya hali ya mvutano kuendelea kuhatarisha usalama licha ya jitihada za kuandaa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya serikali na majeshi ya uasi.
Kikosi hicho kikitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kilikuwa cha kwanza kikiwa na askari takribani elfu 6 walioidhinishwa na Baraza la Usalama kuimarisha usalama huko sudan kusini.
Umoja wa Mataifa ulitahadharisha hatari iliyopo huku bado idadi kubwa ya miili ambayo haikuweza kukusanywa imeonekana katika kambi za umoja wa mataifa.

Hapo jana duru ziliarifu kuwa Waasi wanaomuunga mkono aliyekuwa Makamu wa rais wa Sudan Kusini Salva Kiir wanajiandaa kukabaliana na vikosi vya serikali katika jimbo la Unity lenya utajiri wa Mafuta.

Haya yanafanyika kipindi hiki viongozi wa nchi wanacaham wa IGAD wakikutana jijini Nairobi nchini Kenya kujaribu kupata suluhu kuhusu hali ya usalama na kisiasa nchini Sudan Kusini.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company