Mangariba 38 waukeketaji wakamatwa Moshi Klimanjaro

NA BBC


Ukeketaji hufanywa katika sehemu nyingi Tanzania licha ya kuharamishwa

Maafisa wakuu mjini Moshi Tanzania, wamewakamata wanawake 38 waliopatikana wakiwakeketa wasichana katika eneo hilo.

Haijulikani idadi ya wasichana waliokuwa wanakeketwa , lakini ripoti zinasema kuwa walikuwa kati ya umri wa miaka 3 na 16.
Ingawa ukeketaji ambao umeharamishwa huendelezwa katika sehemu nyingi za Mara na Dodoma nchini Tanzania , hilo sio jambo la kawaida mjini Moshi.

Inaarifiwa wanawake hao walikamatwa Jumapili walipokuwa wanacheza dansi ya kitamaduni wakiwazingira wasichana ambao ndio walikuwa wamekeketwa tu.

Baadhi ya wasichana inaarifiwa bado walikuwa wanavuja damu na wengine wakiwa wanauguza majeraha.

Ukeketaji umeharamishwa nchini Tanzania tangu mwaka 1998 ingawa bado unaendelezwa katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo.

Inakisiwa asilimia 15 ya wasichana pamoja na wanawake wamekeketwa nchini humo.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company