Mkalimani wa mazishi ya Mandela alazwa



Thamsanqa Jantjie, mkalimani wa lugha ya ishara

Mkalimani wa lugha ya ishara katika siku ya mazishi ya kitaifa, ya aliyekuwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, amelazwa katika hospitali ya magonjwa ya ya akili.

Mkalimani huyo anashutumiwa kutoa ishara ambazo hazikuendana na kile kilichokuwa kikiongelewa.

Thamsanqa Jantjie "anaweza kuwa na matatizo", amekaririwa mke wake Siziwe akisema hayo.

Wataalam wa lugha ya ishara wamemshutumu kwa kutoa tafsiri potofu wakati viongozi mbalimbali wakitoa hotuba zao kwenye mazishi ya kitaifa ya Bwana Nelson Mandela wiki iliyopita.

Bwana Jantjie amesema aliumwa ghafla ugonjwa wa schizophrenia.

Amesisitiza kuwa alikuwa ni mkalimani mwenye ujuzi wa kazi hiyo.

Chama tawala cha African National Congress,ANC, amesema imekuwa ikimtumia Bwana Jantjie kama mkalimani wa lugha ya ishara katika matukio kadha siku za nyuma na hakuwahi kulalamikiwa kuhusiana na huduma yake, kwa upande wa ujuzi au maradhi yoyote.

Bwana Mandela alifariki dunia tarehe 5 Desemba mwaka huu akiwa na umri wa miaka 95 na kuzikwa Jumapili.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company