Tume ya Katiba kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Mhe. Rais Desemba 30 2013 katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Hafla ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Mhe. Rais
Tume ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwafahamisha wananchi na wadau wengine wote
kuwa Hafla ya kukabidhi Rasimu ya Katiba kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi itafanyika siku ya Jumatatu, Desemba 30, 2013 katika
Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo pia inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, taasisi za
kidini, asasi za kiraia na wananchi wa kawaida.
Taarifa zaidi kuhusu hafla hii zitatolewa baadaye.
Imetolewa na:
Imetolewa na:
Assaa Rashid,
Katibu,
Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
Dar es Salaam
Desemba 19, 2013.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company