Wananchi Waislamu wa Iran katika mikoa tofauti wameshiriki katika hafla ya kukumbuka mwaka wa 4 tangu yalipojiri maandamano makubwa ya Disemba 30 mwaka 2009 yaliyohitimisha miezi kadhaa ya machafuko ya baada ya uchaguzi wa rais. Watu wengi wamekusanjika katika misikiti na maeneo mengine mjini Tehran na katika miji mingineyo ya Iran ili kukumbuka siku hiyo na kuudhihirishia ulimwengu mshikamano wao kwa taifa na kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Akihutubia huko mjini Isfahan, Hujatul Islam Walmuslimin Ali Natiq Nouri amesema, hamasa ya Disemba 30 ina ujumbe kwa pande tatu, upande wa marafiki, maadui na kwa viongozi wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu. Mwaka 2009 wafuasi wa wagombea wawili walioshindwa katika uchaguzi wa rais walidai kuwa kumetokea udanganyifu na kuanzisha maandamano na ngasia, suala lililopelekea makumi ya watu kuuawa na kujeruhiwa. Ghasia na machafuko hayo yalihitimishwa na maandamano makubwa ya wananchi waliokuwa wakiunga mkono mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu katika siku kama ya leo.